Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam akitoka kituo cha Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akikata tiketi ya mabasi ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika
Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo
kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga naye akiwa mmoja wa wasafiri
wa mabasi hayo. Masauni aliyapanda basi la Mwendo kasi mara baada ya kufanya
ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu
pamoja na usalama wa abiria. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akiigusisha tiketi yake katika mashine ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya
UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam ili mruhusu kuingia ndani
ya stendi hiyo kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho
kuelekea Posta. Mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya
Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akiingia ndani ya Basi la Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo
cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na basi hilo kuelekea
katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya
Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akitelemka katika moja ya mabasi ya
mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam katika kituo cha
Nyerere, Posta. Masauni alipanda basi hilo akitokea Ubungo baada ya kufanya
ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu
pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akiondoka katika Kituo cha Mabasi ya
Mwendokasi cha Nyerere, Posta, mara baada ya kusafiri na usafiri huo akitokea
Ubungo, jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi
Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria.
Katikati ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna,
Mohamed Mpinga Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
***************************
Na Felix Mwagara, MOHA
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameupongeza Mradi wa
Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT wa jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi
waendelee kuyatumia mabasi hayo wanaposafiri sehemu mbalimbali jijini humo.
Mhandisi
Masauni ameyasema hayo jana mara baada ya kusafiri na mabasi hayo kutoka kituo
cha mabasi hayo cha Ubungo mpaka katikati ya jiji kwa lengo la kujionea jinsi
mabasi hayo ya mwendokasi yanavyohudumia abiria pamoja na kuwapa moyo wananchi
kuwa usafiri huo unatumiwa na mwananchi wa aina yeyote.
Akizungumzia
usafiri huo, Masauni alisema mradi huo umerahisisha sana usafiri kwani ametumia
dakika chake akitokea Ubungo hadi Posta katikati ya jiji bila usumbufu wowote,
hivyo mradi huo ameomba uendelee kulindwa pamoja na kutunzwa na UDA-RT na
wananchi wenyewe kwa ujumla.
“Mimi
kwa kweli nimeufurahia sana usafiri huu, Serikali imefanya jambo kubwa sana kwa
wananchi wake, kwa kuwajali wananchi kwa kuuleta mradi huu ambao unarahisisha
safari kwa uharaka zaidi na pia unapendezesha jiji kwa jinsi magari yalivyo
nadhifu,” alisema Masauni ambaye pia alilipa nauli kwa kupanga foleni kama
wananchi wengine wanavyofanya wanapotaka kusafiri na usafiri huo.
Masauni
aliongeza kuwa; “Nimefarijika sana na lugha ya adabu na tulivu ambayo
wanaitumia madereva wa mabasi hayo wanapowatangazia wananchi vituo mbalimbali
vya kushuka na kuingia kwenye mabasi hayo, hii inasaidia kuwa na mawasiliano
mazuri na abiria, pia inaonesha madereva hao wamefunzwa vizuri na wanaipenda
kazi yao.”
Hata
hivyo, Masauni alitoa ushauri kwa uongozi wa mabasi hayo, kuruhusu wananchi
waingie ndani ya mabasi hayo kwa idadi ambayo haitaleta kero kwa abiria wengine
ili kupunguza wingi wa abiria hao kwa lengo la kuepuka mbanano mkubwa wa
abiria.
Pia
aliwataka wananchi wa jiji hilo kuyatunza mabasi hayo, na pia kukubali
maelekezo ya madereva wanapotoa matangazo wanapokuwa safarini kuelekea maeneo
mbalimbali ya jiji.
Naibu
Waziri huyo alipanda mabasi hayo akitokea Ubungo mara baada ya kumaliza ziara
yake ya kushtukiza kwa kutembelea Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kwa lengo la kukagua
mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria wanaosafiri na mabasi hayo. Masauni pia alifanya ziara hiyo ya ghafla kwa
kutembelea Stendi ya Kibaha, mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment