Moja ya Ndege mpya
mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL)
ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20,
2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier
Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili
kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho
akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege
mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya
ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere saa sita na robo juu alama leo
Septemba 20, 2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier
Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye Moja ya
Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege
Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius leo Septemba 20, 2016.
Katibu
Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara
baada ya Moja ya
Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege
Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo
Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo
PICHA NA IKULU
Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
No comments:
Post a Comment