Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akitizama vitabu
wakati akitembelea katika sehemu za
maonyesho zilizoandaliwa kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo
iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja
ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Naibu Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh.
Selemani Jafo akitizama moja ya maonyesho ya
mafunzo yanayotolela kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati
kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika
katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akizungumza katika semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa
vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika
katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo katika picha ya
pamoja na wawakilishi kutoka CHAHITA kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya
hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA)
iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Na Nasra Mwangamilo
Naibu Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jafo amesema
ni muhimu somo la hisabati likatiliwa mkazo na wazazi, wanafunzi na walimu ili
kuwapata wataalamu wabobezi kwenye somo hilo.
Naibu Waziri
aliyasema hayo wakati akitoa hotuba katika ufunguzi wa semina ya mafunzo ya
hesabu iliyoandaliwa na chama hicho itakayoendelea kwa muda wa siku sita katika
moja ya majengo ya ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma .
“Nimefarijika
sana kwa ninyi kunipa fursa kuwa nanyi katika siku ya leo kwani najua lengo
kubwa la semina yenu lakini pia lengo kubwa la chama chenu ni kuhakikisha
taaluma ya hesabu inatamalaki katika nchi yetu ikiwa lengo kubwa ni kupata
wataalamu wazuri waliobobea katika nyanja hii,” alisema Mh. Jafo.
Mh. Jafo
aliongeza kuwa kwa sasa ni muhimu kufanya tathmini ni kwa namna gani wanaweza
kuhakikisha ufaulu wa hesabu unaongezeka kwa wataalamu kuweza kubuni mbinu tofautitofauti za ufundishaji wa
somo hilo na kuhakikisha mbinu hizo zinatawanyika katika maeneo mbalimbali ili
kuwasaidia wanafunzi kupata uelewa katika kulisoma somo hilo.
Akiongea kwa
niaba ya CHAHITA mwenyekiti wa chama hicho Dk. Said Sima alieleza malengo ya
chama hicho kuwa ni kuwaendeleza na kuwapa mafunzo walimu katika vijiji 489 na wilaya zote
nchini ili kuhakikisha wanafundisha wanafunzi somo la hisabati kwa dhana ya
nadharia na vitendo.
Pia Dk. Sima alitoa mapendekezo kwa Mh. Naibu
Waziri ambayo ni kuongezewa malipo kwa
walimu wa somo la hesabu, Serikali kubuni mpango kwa wanafunzi wa elimu ya juu
ya ualimu wa somo la hesabu kuwa wanasaidia kufundisha katika shule za jirani
na vyuo wanavyosoma na kubuni mpango wa walimu wa somo hilo kuwa wanapewa muda
wa ziada wa kuwafundisha wanafunzi.
Chama hicho
ambacho kwa sasa kina miaka 51 tangukilipo anzishwa tarehe 11 ya mwezi wa
kwanza mwak 1966 kimeanza semina hiyo leo ikiwajumuisha walimu wa shule za
msingi na sekondari kutoka ndani nan je ya Dodoma, Walimu kutoka Vyuo vikuu,
Wawakilishi kutoka NACTE na NECTA na
wawakiliski kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT).
No comments:
Post a Comment