Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale(Wa kwanza kulia) akitoa
maelezo ya ramani ya Ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover)
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa( Wa kwanza kushoto) wakati alipokagua
ujenzi huo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (Kulia
kwake) wakati alipokagua ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover,
Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akifafanua jambo mara baada ya
kukagua daraja la wapiti kwa miguu lilopo Buguruni Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale
na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa barabara wa Wizara Eng. Light Chobya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Wananchi mara baada ya kumaliza kukagua daraja la
wapiti kwa miguu lililopo Buguruni Jijijni Dar es salaam.
Picha na Benjamin Sawe -Maelezo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya kikandarasi ya Sumitomo
Mitsui inayojenga mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano
ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara kumaliza ujenzi huo kwa wakati
mradi huo ili kusaidia kupunguza tatizo la msongamano.
Akizungumza mara baada kukagua maendeleo
ya ujenzi wa mradi huo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa
kukamilika kwa mradi huo kutajenga historia nchini kutokana na kuwa ni wa mwanzo kujengwa.
“Nimefurahi kuona mradi huu upo
katika hatua nzuri, naomba mkamilishe mradi huu unakamilika kwa ubora na kwa
wakati ili tatizo la msongamano lililopo katika maeneo haya kupungua au kuisha
kabisa”, amesema Waziri Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemtaka
Mkandarasi kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa
umakini na kwa uangalifu wakati wa kipindi chote cha ujenzi ili kuitokuweza
kusababisha foleni katika eneo hilo.
Aidha, Waziri Mbarawa amewataka
wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili kurahisisha
kazi za ujenzi huo kukamilika kwa wakati na kupata matokeo chanya.
“Nawaomba watanzania wenzangu
kuwa wavumilivu na usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote,
kwani ukamilifu wa mradi huu utasaidia kupunguza tatizo la msongamano katika
barabara hizi”, amefafanua Waziri Mbarawa.
Katika hatua nyingine, Profesa
Mbarawa amekagua daraja la watembea kwa miguu eneo la Buguruni Sheli na
kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitunza daraja hilo ambalo uwepo wake umesaidia
kupunguza ajali katika maeneo hayo.
“Ni matumaini yangu sasa wakazi
wa maeneo haya mtavuka kwa amani kupitia
daraja hili, na ajali zilizokuwa zikitokea maramara hazitakuwepo tena”’, amesema
Profesa Mbarawa.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemuahidi Waziri
huyo kumaliza kwa wakati ujenzi huo na kumhaakikishia Waziri kuwa ujenzi wa
barabara hiyo utakuwa na viwango vilivyo bora.
Mradi wa Tazara Flyover ni msaada
kutoka Serikali ya Japan ambao umegharimu shilingi bilioni 93.4 na unatarajiwa
kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawsiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment