Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani,
Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini
katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya
kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa
Polisi, Mohamed Mpinga. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na
Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unafanyika leo katika Ukumbi wa
wa Mikutano wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Sehemu
ya Wadau na Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini
wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni
(hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala
mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo
unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita. Picha
na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha
Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga akitoa
taarifa ya matukio mbalimbali ya ajali za barabarani nchini katika mkutano wa Wadau
wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani kutoka mikoa yote nchini. Mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali
ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Wapili kushoto ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad
Masauni, na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa
Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa wa Mikutano
wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment