National Arts Council BASATA
Tarehe: 30/09/2016
BASATA Arts
Centre
Tel. 2863748/2860485
Fax:
0255- (022) – 286 0486
Ilala Sharif Shamba
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam
E-mail:basata06@yahoo.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa nchini
linapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza msanii na mbunifu wa Mavazi Mustafa
Hassanali kwa kushiriki kinyanga’anyiro cha Tuzo ya Mavazi ya Afrika Mashariki Kenya
2016 (Kenya Fashion Awards 2016) yaliyofanyika tarehe 03/09/2016 na kupata tuzo
ya Mbunifu Bora wa Mwaka wa Afrika Mashariki.
Baraza linathamini
mchango mkubwa wa Mbunifu huyu wa mavazi katika kuendeleza tasnia ya ubunifu, kwa
kuanzisha Jukwaa la mavazi Afrika Mashariki na Kati, Swahili Fashion week na
maonyesho mengine ya mavazi.
Aidha tuzo hii
itakuwa chachu kwa ustawi wa tasnia ya ubunifu wa mavazi kwa kuwa imedhihirisha
ubora wa kazi za sanaa za Kitanzania katika soko la Kimataifa. Baraza litaendelea
kushirikiana na wabunifu wenye maono na bidii katika kukuza na kuendeleza sanaa
nchini ili kuhakikisha sekta ya sanaa inasonga mbele kwani ni ukweli
usiopingika kuwa tasnia ya sanaa ina mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa
watanzania wengi hususan vijana.
Baraza
linatambua mchango wa Bwana Mustafa Hassanali katika kukuza maendeleo ya ubunifu
na amekuwa akitoa fursa kwa wabunifu wengine wa Tanzania, Afrika Mashariki na
Afrika kwa ujumla. Baraza linathamini na linatoa pongezi kwa Bwana Mustafa
Hassanali kwa kazi nzuri anayoifanya.
SANAA NI KAZI
TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA
No comments:
Post a Comment