Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akikabidhiwa
msaada na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akiongea na
wajumbe kutoka Burundi na Tanzania wakati wa kukabidhi msaada kutoka nchini
Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Ujumbe wa Burundi uliongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine
Nzeyimana (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto
(kushoto).
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana akiongea na wajumbe
kutoka Tanzania na Burundi wakati wa kukabidhi msaada kwa lengo la kuwasaidia
waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kushoto ni Waziri wa Afrika
Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na wa kwanza kulia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwakaribisha wajumbe kutoka Burundi na Tanzania
wakati wa mkutano kabla ya kukabidhi msaada kwa lengo la kuwasaidia waathirika
wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Afrika
Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana na katikati
ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan
Kolimba.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto)
akifurahia jambo na Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (katikati) mara baada ya kukabidhi msaada kutoka
nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani
Kagera. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya.
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine
Nzeyimana (katikati) akifafanua jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) mara baada ya
kukabidhi ya kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia
waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya
Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya.
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine
Nzeyimana (kushoto) akifafanua jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia) mara baada ya
kukabidhi ya kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia
waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa
Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana
(wa kwanza kulia) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba (wa pili kulia).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba akimaribisha
Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye mara baada ya
kuwasili mpakani mwa Tanzania na Burundi
katika eneo la Kabanga wilayani Ngara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba akimaribisha
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine
Nzeyimana baada ya kuwasili mpakani mwa Tanzania na Burundi katika eneo la
Kabanga wilayani Ngara.
Viongozi kutoka Serikali za Tanzania na Burundi wakielekea kwenye eneo
yaliposimama malori yaliyobeba shehena ya vyakula vya msaada vilvyotolewa na
serikali ya Burundi ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Viongozi kutoka Serikali za
Tanzania na Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na madereva wa malori
yatakayosafirisha shehena ya vyakula vya msaada vilivyotolewa na serikali ya
Burundi ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Wa nne
kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba na Waziri wa Afrika Mashariki kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (wa tano kutoka kushoto).
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO,
Ngara, Kagera)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Ngara, Kagera.
Serikali
ya Tanzania imepokea msaada wa tani 183 za vyakula mbalimbali kutoka Serikali
ya Burundi kwa ajili ya kuwafuta machozi waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea
mkoni Kagera mapema mwezi huu na kuathiri maisha ya wakazi wa mkoa huo.
Makabidhiano
ya msaada wa vyakula hivyo kutoka nchini Burundi yamefanyika mpakani mwa
Tanzania na Burundi katika eneo la Kituo cha Ushuru cha Pamoja (OSBP) cha Kabanga
wilayani Ngara ambapo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakati Burundi iliwakilishwa
na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na Waziri wa Mambo ya
Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye.
Akikabidhi
vyakula hivyo, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa Serikali ya Burundi na Warundi
wote walipatwa na mshtuko mkubwa na majonzi baada kusikia taarifa ya maafa
yaliyowatokea ndugu zao wa mkoani Kagera.
“Kwa
Kirundi tunasema, “Umubanyi niwe muryango” ikimaanisha jirani yako ni ndugu
yako, kwa maana hiyo imekuwa ni wajibu kwa Serikali ya Burundi kuagiza
wawakilishi wake ili waweze kufika hapa nchini Tanzania mkoani Kagera kuwaona
ndugu zetu Watanzania na kuwapa pole”.
Waziri
Bi. Leontine aliendelea kusema “Ndio maana tumekuja na kifurushi kidogo tu ili
tuweze kuwaliwaza ndugu zetu waliofikwa na matatizo hayo” alisema Waziri Bi.
Leontine
Waziri
Bi. Leontine alivitaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na mchele tani 100, mahindi
tani 50, sukari tani 30 na majani ya chai tani 03.
Akizungumzia
suala la mahusiano ya Tanzania na Burundi, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa
udugu uliojengeka baina ya nchi hizo mbili na wananchi wake ni wa kihistoria,
si wa leo au wa jana na kusema Serikali yake inadhamira ya kuendeleza udugu huo
vizazi na vizazi huku akiamini Tanzania nayo ina dhamira hiyo hiyo.
Akitoa
shukrani baada ya kupokea msaada huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba ameishukuru Serikali ya
Burundi kwa msaada waliotoa kwa Tanzania na kuongeza kuwa msaada waliotoa ni
kielelezo cha mahusiano ya karibu na ya kidugu baina ya nchi hizo mbili na watu
wake.
Pia
Naibu Waziri Dkt. Suzan amewataka viongozi wa Serikali ya Burundi wafikishe
salamu na shukrani za dhati za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza na
kuwathibitishia kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi
hizo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambao ndio umeathirika na tetemeko hilo Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambaye pia ni Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa mkoa
huo ameihakikishia Serikali ya Burundi kuwa msaada walioutoa utawafikia
walengwa kama ilivyokusudiwa.
Msaada huo
uliotolewa na Burundi umekuwa ni mwendelezo wa misaada inayotolewa na nchi za
Afrika Mashariki kwa Tanzania kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Septemba
10 mwaka huu na kuathiri mikoa ya kanda ya ziwa.
Burundi
imeungana na nchi za Uganda na Kenya kwa kutoa misaada kwa waathirika wa
tetemeko hilo ambapo September 17 mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokea
mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki 2 ambazo ni sawa na
takribani Shilingi za Kitanzania milioni 437 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya
Uganda Yoweri Kaguta Museveni na mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye
thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya
Kenya Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
Mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment