Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(aliyevaa tai) akielekea Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es
Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi
mabovu pamoja na usalama wa abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi ya
Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba za usajili
T419 BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga
kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza
kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akiwauliza abiria wa Basi la Harambee linalofanya safari zake Dar es Salaam
kwenda Arusha, maswali mbalimbali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wakati
wanaposafiri. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi
yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akikagua mikanda katika Basi la Shambalai wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto) akioneshwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu
Kamishna, Mohamed Mpinga, tairi la Basi la Shambalai ambalo halina ubora kwa ajili
ya kusafirisha abiria. Hata hivyo Masauni aliagiza basi hilo lizuiwe kufanya
safari na pia kuchukuliwa hatua kali kwa Mmiliki wa basi hilo pamoja na Dereva.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(aliyevaa tai) akizungumza na madereva wa Basi ya mikoani pamoja na wa magari madogo
ya mizigo yanayopaki Stendi Kuu Ubungo, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka
madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani. Hata hivyo, madereva hao
walilalamika kuwa hawana mikataba ya kazi zao. Masauni alifanya ziara ya
kushtukiza katika Stendi hiyo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(katikati) akishuhudia Dereva wa Basi la Tahmeed (kulia) akipimwa kilevi na Trafiki
Nuru Mvungi kabla ya Basi lake kuruhusiwa na safari. Masauni alifanya ziara ya
kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es
Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na waandishi wa habari, Picha ya Ndege Kibaha, Pwani, mara baada ya
kukamilisha ziara yake ya kukagua mabasi mabovu na usalama wa abiria. Masauni
alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani,
Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Kulia ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto) akihoji usalama wa mtoto baada ya kugundua siti moja kukaa watoto
wawili jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya
kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es
Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa
mabasi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto) akiwasalimia wananchi wa Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani mara
baada ya kumaliza ukaguzi wa mabasi mabovu pamoja na madereva ambao hawana
leseni. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi
yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya
Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
*****************************************************************************
Na Mwandishi Wetu, MOHA
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amefanya ziara ya
kushitukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na
Stendi ya Kibaha, mkoani Pwani.
Katika
ziara hiyo, alilizua basi la Shambarai lenye namba za usajili T419 BUF pamoja
na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga kutokuendelea na
safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza kuhatarisha
maisha ya abiria.
Masauni
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani akiwa na Katibu wa
Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu
Kamishna, Mohamed Mpinga, aliwasili katika Stendi hiyo ya Ubungo saa 2:16
asubuhi na kuanza ziara hiyo ambayo aligundua baadhi ya mabasi yaendayo mikoani
hayana viwango na ubora wa kusafirisha abiria.
Aidha,
Masauni alitoa agizo kwa askari wa usalama barabrani pamoja na viongozi walioko
katika kituo hicho, kuboresha mfumo wa ukaguzi wa mabasi hayo kuwa wa kiwango
kinachoridhisha ili kuzidi kupunguza ajali za barabarani pamoja na kuzuia
baadhi ya mabasi yaliyoonekana kuwa na ubovu zaidi kufanya safari ndefu lakini
pia kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wamiliki wa mabasi hayo na madereva wake.
Katika
ziara hiyo Masauni ametoa wito kwa abiria kutokua sehemu ya kusababisha ajali
kwa kutaka dereva kukimbia sana lakini pia kutoa ushirikiano hasa katika kutoa
taarifa polisi pamoja na Chana cha Kutetea Abiria (CHAKUA) juu ya madereva
wanaoendesha kwa spidi ambayo ni hatari kwa maisha yao lakini pia kuepuka
kupanda magari yasiyokuwa na mikanda, na viti vilivyolegea.
Lengo
la Serikali na viongozi mbalimbali ni kuhakikisha ajali za barabarani
zinapungua ama kuisha kabisa hivyo haiwezi kufumbia macho makosa yanayoweza
kusababisha ajali, “Pesa inatafutwa lakini roho haitafutwi hivyo ni vema kuwa
makini barabarani, alisema masauni na kufafanua kuwa;
“Mkakati
wa kuzuia ajali ni kuwa na mfumo endelevu wa kuzuia ajali za barabarani na si
ya muda mfupi hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi
havitakoma kuongeza nguvu ili kumaliza tatizo hilo na kuwachukulia hatua kali
wamiliki na madereva wanaoendesha mabasi mabovu hivyo kuhatarisha usalama
barabarani.”
Aidha,
Masauni amewataka madereva wote pamoja na makondakta kuhakikisha abiria wote
wamefunga mikanda kabla ya kuanza safari pia kuendesha kwa kuzingatia alama za
barabarani ili kuzidi kupunguza ajali kwani dhamana ya maisha yao iko mikononi
mwao.
Idadi
kubwa ya abiria kwenye vituo hivyo vya mabasi wameonesha kuridhishwa na mwendo
wa mabasi yanapokua barabarani lakini wameiomba Serikali iendelee kufuatilia
madereva wanaokiuka sheria za usalama wa barabarani.
No comments:
Post a Comment