CONGO TUTAWAZIKA HAPA...
Ndivyo anavyoonekana
kusema Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto)
akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya
miaka 17 - Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse
Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo. Uwanja huo ulioko kwenye Makutano ya
Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville ndio utakaotumika kwa ajili
ya mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya
Tanzania na Congo, Jumapili Oktoba 2, 2016.
Huyo
ndiye Muhsin Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya
Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo
kuonyesha uwezo wake uwanjani pindi anapoingia kipindi cha pili kuokoa jahazi.
Akikosa kufunga huwa ni kama bahati mbaya.
Kiungo wa
Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys,
Kelvin Nashon ‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais
wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Beki wa
kushoto wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti
Boys, Nickson Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais
wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Libero wa
Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ally
Msengi (Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah
akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo
wa Jumapili.
Baadhi ya
vigogo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti
Boys, kutoka kushoto ni Dk. Gilbert Gilbert Kigadye, Mratibu wa timu,
Pelegrinus Rutayuga na Dk. Sheicky Mngazija wakifuatilia mazoezi hayo kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla
ya mchezo wa Jumapili.
Kipa Na.
1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys,
Ramadhani Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse
Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
No comments:
Post a Comment