|
Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akizungumza na wakazi wa Kawe kuhusu kampeni ya VIWANDA NI FURSA.
|
Katika
kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuifanya Tanzania inakuwa
nchi ya viwanda, Mkurugenzi wa Kampuni ya HiTECH International, Paul
Mashauri ameanzisha kampeni mpya ya VIWANDA NI FURSA ambayo itatoa elimu
kwa wananchi pamoja na kutoa mikopo ya mashine za viwanda vidogo vidogo
kwa wajasiliamali.
Akielezea
kampeni hiyo wakati akifanya semina kwa wakazi wa Kawe, Mashauri
alisema kuwa ameanzisha kampeni hiyo ili kutoa elimu kwa wananchi lakini
pia kuwapa mikopo ya mashine kwani watu wengi wanatamani kufanya
biashara lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukosa mtaji wa kufanya
biashara.
Alisema
kuwa ili nchi kuwa kufanikiwa kwa kuwa na uchumi mkubwa na kuwa na
maendeleo kwa wananchi wake ni lazima iwe na viwanda vingi ili kuwepo
ajira za kutosha na shughuli za maendeleo hivyo kupitia kampeni hiyo
itaweza kubadili maisha ya watanzania wengi ambao tayari walikuwa
wameanza kupoteza matumaini ya kufanikiwa kimaisha.
|
Mkurugenzi
wa Kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akieleza wakazi wa
Kawe jinsi wanavyoweza kubadili maisha yao kwa kufanya biashara na jinsi
kampuni yake ya HiTECH inaweza kuwapa mkopo. |
"Kampuni
ya HiTECH imeanzisha kampeni hiI na itafanyika nchi nzima, serikali
tayari imekubali tuifanye kimechobaki ni wananchi wenyewe, tutatoa
mikopo ya mashine kwa watakaohitaji na watarudisha kwa riba ndogo ya
asilimia 10,
"Ukienda
nchi ambazo zimeendelea kama China kuna viwanda vingi, na watu wanajua
kiwanda mpaka uwe na eneo kubwa wakati watu hata majumbani wana viwanda
na wanazalisha, ni muda sasa watanzania kuchangamkia nafasi hii ambazo
HiTECH International imeitoa," alisema Mashauri.
Nae
Diwani wa Kawe, Ruta Rwakatare alimpongeza Mashauri kwa uamuzi wa kutoa
mikopo kwa wananchi ambao wana malengo ya kufanikiwa kwa kufanya
biashara na anaamini kuwa hiyo itakuwa njia moja wapo ya kumaliza vijiwe
vya vijana ambao hawafanyi kazi.
"Mimi
sipendelei kuona vijana wanakaa tu vijiweni, na sio kwamba wanapenda
ila tu sababu hakuna kazi lakini kupitia kampeni ya Paul Mashauri
itaweza kuwasaidia kuacha tabia hizo na kuanza kufanya kazi
zinazowaletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment