Mkurugenzi wa ulinzi na
usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na
waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na
uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud.
Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wa leo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Mkoani Tanga
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano huo
Waandishi wa Habari wa Mkoani Tanga wakichukua habari leo
PRO wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA)Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari wa mkoani Tanga.
MAMLAKA ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi
Kavu (SUMATRA) imekusudia kuanzisha mpango mkakati maalumu wa udhibiti uchafuzi
wa mazingira baharini (NMOSCRP) unaosababishwa na umwagaji wa mafuta unaofanywa
bila ya kufuata taratibu za mazingira zilizowekwa na kuharibu mazingira.
Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama wa vyombo vya majini Taifa Capt Mussa Hamza wakati akizungumza na waandishi
wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wiki ya bahari dunia inayofanyika
Kitaifa Mkoani Tanga kwenye viwanja vya Tangamano kesho Jumanne.
Ambapo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Makame Mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yatakayokwenda
sambamba na maonyesho mbalimbali na warsha itakayofanyika Septemba 28 mwaka
huu.
Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa biashara ya
usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari wame lazimika kuanzisha mpango huo ili
kukabiliana na uchafuzi huo ambao unaweza kuchangia utoekaji wa viumbe vya
vilivyopo.
Aidha alisema kuwa kutokana na uchavuzi huo wa
mazingira uliopitiliza unachangia kwa kiasi kikubwa kuhatarisha mazilia ua
samaki katika bahari na viumbe vingine vilivyomo baharini.
Alisema Tanzania imeingia katika shughuli za
uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo usafiri mkubwa wa mafuta ni kwa njia ya
bahari hali ambayo inalazimika kuanzisha sheria maalumu ambayo inaweza kulinda
mazingira ya bahari.
“Hakuna vyombo vinavyokuwa na uwezo wa
kubeba mizigo mikubwa kama vyombo bya baharini hivyo imetulazimu kuanzisha
mpango maalumu ambao tunategemea kesho kuuzindua ili kuweza kukabilia na
uchavuzi wa mazingira katika bahari yetu ya Hindi”Alisema.
Hamza
alitumia fursa hiyo kueleza kuwa miongoni mwa sababu za kufanya maadhimisho
hayo Kitaifa Mkoa wa Tanga ni kutokana na mkoa huo kuingia katika mradi mkubwa
wa usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bomba kutoka nchini Uganda hadi bandari
ya Tanga ambapo kutakuwepo na fursa kubwa ya kuitangaza Tanga kwa wawekezaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya usafirishaji wa
Majini Zanzibar (ZMA) Suleiman Masoud alisema kufanyika kwa maadhimisho hayo
katika mkoa wa Tanga ni tija kwa bandari ya Tanga,kupitia maadhimisho hayo
lengo ni kuitangaza bandari hiyo kwa wafanya biashara wakubwa ndani na nje ya
nchi.
Alisema Tanga inaweza kuwa ni sehemu kuu
ya kitovu cha biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari na hata
nchi kavu ikiwa itawekewa mipango madhubuti ya kuifufyua bandari ya Tanga.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment