Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akimkabidhi fedha taslimu Shilingi 1,119,000, Msimamizi wa Kituo cha Watoto
Yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa
ajili ya kusaidia majukumu mbalimbali ya ulezi wa watoto hao. Fedha hizo
zilitolewa na Masauni pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo kwa lengo la kusaidia
kituo hicho. Pia Baraza hilo lilitoa mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu
la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na fulana 100. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto) akimkabidhi misaada mbalimbali, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima
cha Moyo wa Huruma kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa ajili ya
kusaidia watoto hao. Pia Masauni alimkabidhi msimamizi huyo wa kituo mchele
gunia moja, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11, fulana 100 pamoja na
fedha taslimu Shilingi 1,119,000 ambazo zilitolewa na wajumbe wa Baraza hilo.
Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba
mtoto) na Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna,
Mohamed Mpinga (kulia) wakiwa na baadhi ya watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa
Huruma cha mjini Geita, mara baada ya Masauni kukabidhi fedha taslimu shilingi
1,119,000 pamoja na vyakula kwa kituo hicho ambapo misaada hiyo ilitolewa na
Baraza la Usalama barabarani ambalo linaadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama
mjini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
(kulia) akizungumza na Watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma kabla ya
kuwakabidhi misaada mbalimbali ambayo aliwaongoza Wajumbe wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani kukusanya misaaida mbalimbali. Misaada hiyo iliyotolewa ni fedha
taslimu shilingi 1,119,000 pamoja na mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu
la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na fulana 100. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni
(aliyembeba mtoto), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel
Kyunga (kulia kwa Masauni), pamoja na
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wakiwa katika picha ya pamoja
na Watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma cha mjini Geita, wakati Mwenyekiti
huyo wa Baraza pamoja na wajumbe wake kukitembelea kituo hicho na kukabidhi
misaada mbalimbali. Tukio hilo lilifanyika mara baada ya Masauni kuizindua Wiki
ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo inaadhimishwa Kitaifa mjini Geita. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni amewaomba
Watanzania kuweka utamaduni wa kuvisaidia vituo vya watoto yatima nchini
ili kuwasaidia watoto hao ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Masauni
alisema hayo mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali katika Kituo
cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma ambacho kinasimamiwa na Kanisa
Katoliki mjini Geita.
Naibu
Waziri huyo ambaye yupo mjini humo kwa ajili ya kuadhimisha Wiki ya
Nenda kwa Usalama ambayo aliizindua jana Septemba 26 katika Viwanja vya
CCM Kalangalala ambapo inafanyika kitaifa mjini humo.
Masauni
aliwaongoza Wajumbe wa Baraza la Taifa kukusanya fedha taslimu shilingi
1,119,000 kituoni hapo ambapo licha ya fedha hizo Baraza hilo lilitoa
misaada mbalimbali ikiwemo mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu la
mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na fulana 100, alisema
lazima Watanzania tuweke utamaduni wa kuvichangia vituo vya watoto
yatima.
“Natoa
pongezi kwa uongozi wa Kanisa Katoliki kwa kukisimamia kituo hiki,
kuishi na watoto wetu, kuwahudumia vizuri, kwa kweli hili linapaswa
kupongezwa. Tupo hapa Geita kwa ajili ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani lakini tumeguswa na kuamua kutoa michango mbalimbali
kwa kituo hiki, na tunawataka Watanzania pia waweke utamaduni huu wa
kuvisaidia vituo hivi katika sehemu mbalimbali waliopo nchini,” alisema
Masauni.
Masauni
aliongeza kuwa, Serikali ya Rais John Magufuli ipo kwa ajili ya
kuwasaidia Watanzania wote, kama mnavyoona katika elimu imeweka
kipaumbele ili watoto wetu waweze kusoma katika mazingira mazuri.
Kwa
upande wake Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu
Kamishna, Mohamed Mpinga alitoa pongezi kwa Naibu Waziri Masauni
kwakuwaongoza kutoa misaada hiyo kwa kituo hicho.
“Mwenyekiti
wa Baraza ametuonyesha njia, ametuongoza na kuweza kufanikisha zoezi
hili la uchangiaji, tunamshukuru sana kwa uamuzi huo wa busara wenye nia
njema ya kuwasaidia watoto wetu.” Alisema Mpinga.
Aidha,
Mlezi wa Kituo hicho, Sista Adalbera Mukure alimshukuru Masauni pamoja
na Wajumbe hao kwa moyo wao wa kukichangia kituo hicho, pia aliishukuru
Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanya mambo mengi yanayoonekana.
“Tunafuraha
sana kwa ujio wenu, tunashukuru sana kwa misaada mbalimbali mlioitoa,
na pia tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya mambo mengi
yanayoonekana, sisi tunasaidia serikali hii kwa sala zetu, hatupo katika
siasa,” alisema Sista Mukure.
No comments:
Post a Comment