Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista
Muhagama akitembelea eneo la kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa
kujionea ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulivyoathari mazao ya ndizi
na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera na kuwaomba wananchi wa mkoa huo
wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista akiwa ziarani wilaya ya
Kyerwa na kujionea mazo la viazi ambalo pia linaweza kulimwa wilayani humo.
(Picha na Eleuteri Mangi,
MAELEZO, Kyerwa, Kagera).
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO,
Kyerwa
Ukame unaotokana na mabadiliko ya
tabia nchi ulioathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera umemlazimu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu
Jenista Muhagama kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao
mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.
Athari hiyo ya ukame imemlazimu Waziri
Mhagama kuwataka wananchi wa wilaya hiyo na mkoa wa Kagera kwa ujumla w0aanze kulima
mazao mengine yanayokomaa kwa muda mfupi yaweze kuwapunguzia adha ya upungufu
wa chakula unaotokana na kutegemea zao la ndizi pekee.
Akiwa katika kijiji cha Ntare kata
ya Itera wilayani Kyerwa Waziri Mhagama aliongea na wananchi wa kata hiyo ambapo
alisema “Mabadiliko ya tabia nchi ni makubwa, msiendelee kutegemea zao moja tu
la chakula la ndizi, ni lazima mkubali sasa tuende kwenye mazao mengine ya
chakula, limeni mihogo, limeni mahindi. Nendeni kwenye mazao yanayokomaa kwa
muda mfupi, vinginevyo tukisema kila kila mwaka tuendelee kutegemea kahawa na ndizi
kwa hali ya hewa ilivyo sasa tutaendelea kukosa chakula”.
Waziri Mhagama aliyataja mazao
hayo kuwa yanaweza kukomaa kwa muda mfupi kuanzia miezi mitatu ndiyo yanaweza
kuwa mkombozi wa katika kukabiliana na upungufu wa chakula na kuwahakikishia
wananchi chakula cha kutosha hatua ambayo itawafanya waendelee na shughuli
zenye tija kwa maendeleo yao.
Mkulima wa kata hiyo Shakiru Issa
anathibitisha kuwa upo uwezekano wa kulima mazao mengine zaidi ya ndizi na
kahawa ambayo yanamuongezea kipato ambapo yeye analima pia zao la viazi
mviringo kwa ajili ya chakula pamoja na kuuza hatua inayomsaidia kumuongezea
kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.
Ili kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi Waziri Mhagama amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha tabia ya
kuchoma mapori moto mara moja kwa kuwa tabia hiyo huhatarisha maisha ya watu,
kupoteza mazao shambani,miti na hifadhi ya misitu ambayo ndiyo kivutio kikuu
cha mvua.
Aidha, ziara hiyo wa Waziri
Mhagama imekuwa faraja kwa wananchi wa Kata ya Itera ambapo amemwagiza
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi
Msuya aende kufanya tahmini ya hali ukame ilivyo athiri wilaya hiyo na kutoa
taarifa mapema iwezekanavyo.
Katika kuhakikisha upatikanaji wa
chakula cha kutosha wilayani Kyerwa, Waziri Mhagama ametoa wito na kumuagiza Mkuu
wa Wilaya hiyo Kanali Mstaafu Shaban Lissu pamoja kulima zao la ndizi, aanza haraka
kampeni ya kuwahamasisha wananchi hao kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi
ambayo yataweza kuwapatia chakula cha kutosha kwa mahitaji yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment