Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ametoa
ofa kwa wananchi kujumuika pamoja leo Septemba 18, 2016 katika mchezo wa
mpira wa miguu utakaozikutanisha timu za vijana taifa za Tanzania na
Congo-Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe, jijini Dar
es Salaam.
Timu
hizo zitakutana kweye mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya
miaka. Zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na
timu itafayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa
fainali hizo.
Nape
alitoa ofa hiyo tangu jana Septemba 17, 2016 na leo asubuhi Septemba
alipata kifungua kinywa na wachezaji wa Serengeti Boys ambako alitoa Sh
200,000 kwa kila mchezaji zilizotokana na kundi linalosapoti Serengeti
Boys ambao walichangia Sh 2,600,000 wakati nyingine zilitoka kwa wadau
wengine.
Nape
ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha hizo
kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake
itakuwa Sh 5,000,000. “Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa
fedha zaidi, kwa hiyo Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo
mbele ya Watanzania watakaoingia uwanjani bure.”
Kuingia
bure kesho ni ofa iliyotolewa na Nape ambako Rais Jamal Malinzi
amemshukuru Nnauye ambaye ni Mbunge wa Mtama kwa ofa hiyo ambayo
imelenga kutoa hamasa kwa Watanzania kwenda kushangilia timu yao.
Katika
mchezo huo ambao Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, amesema kwamba amemaliza
kila kitu na kwamba anasubiri Watanzania kuja uwanjani leo kuishangilia
timu yao, utachezwa na waamuzi kutoka Shelisheli ambako mpiga kipenga
atakuwa Nelson Fred akisaidiwa na Hensley Petrousse na Stive Marie
wakati mwamuzi wa akiba akiwa Allister Barra. Kamishna wa mchezo atakuwa
Gladmore Muzambi kutoka Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment