Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo mitano ya Mzunguko wa Nne.
Miongoni
mwa michezo hiyo, itakuwa ni ile ya upinzani wa jadi kati ya JKT Ruvu
itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko
Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Stand United
kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Mbali
ya michezo hiyo, pia Young Africans itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya
Songea kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wakati Azam FC ambayo
itakuwa mgeni tena kwenye Uwanja wa Sokoine ikicheza na Mbeya City na
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Ndanda itaikaribisha Kagera Sugar ya
Kagera.
Ligi
hiyo itaendelea Jumapili Septemba 11, 2016 kwa Simba kuikaribisha
Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, lakini
uliokuwa uzikutanishe timu za African Lyon na Mbao hapo kesho umesogezwa
mbele hadi Jumatatu Septemba 12, 2016. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa
Uhuru baada ya African Lyon kubadili uwanja kutoka Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume.
No comments:
Post a Comment