Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya
Na BEATRICE LYIMO, MAELEZO, DODOMA
Serikali
imekuwa ikifanya utafiti juu ya gharama halisi na maisha ya wanafunzi
wa vyuo vikuu ambazo hujumuisha gharama za chakula na malazi vyuoni.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi
Stella Manyanya alipokuwa akijibu swali la Mhe. Zainab Katimba (Viti
Maalumu) lililohusu mpango wa Serikali kuongeza fedha kwa wanafunzi hao.Naibu
Waziri Mhandisi Manyanya amesema kuwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo
ya wanafunzi wa elimu ya juu ilifanya utafiti katika vyuo vyote nchini
ili kujua gharama halisi za chakula na malazi ambapo utafiti huo
umebainisha kuwa gharama hizo ni kati ya 8,000 na 8,500 kwa siku.
Aidha,
ameongeza kuwa utafiti huo hufanywa kila baada ya miaka miwili, hivyo,
Wizara yake itafanya utafiti mwingine ili kubainisha gharama halisi za
chakula na malazi ambapo matokeo ya utafiti huo yatatumika kupanga
viwango vya fedha atakazolipwa mwanafunzi kwa kuzingatia gharama halisi
pamoja na upatikanaji wa fedha.
Mbali
na hayo, akijibu swali la Mhe. Zainabu Mwamwindi lililohusu mpango wa
Serikali kuviwezesha vyuo vikuu nchini kufanya utafiti Mhandisi Manyanya
amesema kuwa Serikali imekuwa ikitenga fedha hizo kupitia Mfuko wa
Taifa wa Uendeshaji wa Sayansi na Tekinolojia (MTUSATE) unaoratibiwa na
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
“Fedha
za utafiti kutoka kwenye mfuko huo zimekuwa zikitumiwa na watafiti wa
ndani ya nchi wakiwemo watafiti kutoka vyou vikuu ambapo utaratibu ni
kwamba miradi hii ya utafiti hufadhiliwa kwa misingi ya ushindani
kuoitia ubora wa maandiko ya miradi ya utafiti”, amefafanua Mhandisi
Manyanya.
Mbali
na hayo vyuo vikuu vyote nchini vinatakiwa kutenga fedha kupitia bajeti
zao pamoja na kutafuta wafadhili na wadau wa maendeleo kwa ajili ya
kuendesha shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kufanya utafiti.
No comments:
Post a Comment