Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji
Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi
ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam jana. Wa kwanza upande wa kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji
Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi
ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa na Mkurugenzi wa
Sera na Mipango wizarani hapo, Haji Janabi. Wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi
wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba, anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha,
Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba akijitambulisha
kabla ya kuanza kikao cha Watendaji Wakuu wa NIDA pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kilichoitishwa na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) na kufanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na anayefuata ni Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza
jambo katika kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala
mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya NIDA na Wizara kiujumla. Kikao hicho
kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Wa tano kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
*****************************************************************************
No comments:
Post a Comment