Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia
aliyevaa kiraia) akiingia ndani ya Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini
Moshi. Rwegasira amefanya ziara kwa kukitembelea kiwanda hicho kwa lengo la
kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza. Picha zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(kushoto) akimsalimia Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo wakati Kiongozi huyo wa Wizara
alipowasili katika ofisi za Magereza Mkoa, mjini Moshi.
Fundi
wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi, Hashim Rashid akimuonyesha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kushoto) jinsi buti la Jeshi linavyotengenezwa ndani ya kiwanda
hicho.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akiangalia buti la Jeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga,
mjini Moshi. Kiwanda hicho kinatengenezwa viatu vya aina mbalimbali. Kushoto ni
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Venance Kayombo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza
na Maafisa wa Magereza, Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mara
baada ya kumaliza kukitembelea Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi.
Rwegasira alikipongeza kiwanda hicho na kulitaka Jeshi la Magereza kuongeza
juhudi zaidi katika uzalishaji wa viatu.
Mkuu
wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro, Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Anderson James akimpa zawadi ya viatu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia)
mara baada ya kufanya ziara ya kukikagua kiwanda hicho pamoja na kujifunza
jinsi ya utengenezaji wa viatu unavyofanyika. Kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoani
Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment