- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kulia) wakipongezana na Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels (wa pili kushoto) mara baada ya uzinduzi wa 'NMB Pamoja Account'. wengine ni Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) na Mkurugenzi wa Kiufundi wa Shirika la Care, Oliva Kinabo (kushoto) wakishuhudia.
- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa bidhaa ya 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki hiyo na Shirika la Care nchini Tanzania. Kushoto akimsaidia ni Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels.

- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels (kushoto) kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki hiyo na Shirika la Care nchini Tanzania. Kulia ni Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela akishuhudia.
- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa bidhaa ya 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki hiyo na Shirika la Care nchini Tanzania. Kushoto akimsaidia ni Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels.
- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jana jijini Dar es Salaam kabla ya uzinduzi wa 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki ya NMB pamoja na Shirika la Care nchini Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels.
- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam kabla ya uzinduzi wa bidhaa ya 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki ya NMB pamoja na Shirika la Care nchini Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels na kulia ni Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela.
- Baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya kwanza vilivyonufaika na bidhaa mpya ya 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki hiyo na Shirika la Care nchini Tanzania.
- Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels akizungumza jijini Dar es Salaam kabla ya uzinduzi wa 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki ya NMB na Shirika la Care nchini Tanzania. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela.
- Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kabla ya uzinduzi wa bidhaa ya 'NMB Pamoja Account'. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker.
- Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kabla ya uzinduzi wa bidhaa ya 'NMB Pamoja Account'. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker.
- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa bidhaa ya 'NMB Pamoja Account' iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Benki hiyo na Shirika la Care nchini Tanzania. Kushoto akimsaidia ni Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels.
- Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Care nchini Tanzania, Paul Daniels (wa tatu kushoto) wakipiga picha na wawakilishi wa vikundi vya kwanza vilivyonufaika na bidhaa ya 'NMB Pamoja Account'. Wengine ni Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) na Mkurugenzi wa Kiufundi wa Shirika la Care, Oliva Kinabo (wa pili kushoto) wakishuhudia.

BANKI ya NMB kwa kushirikiana na Shirika la Care imeanzisha akaunti ya kikundi ijulikanao kama 'NMB Pamoja Account' itakayowasaidia wajasiliamali kwenye vikundi vidogo vidogo kuifadhi fedha zao salama na kuzitumia muda wowote bila vikwanzo tofauti na hapo awali ambapo vikundi hivyo vilikuwa vikiifadhi kwenye maboksi na chini ya mito ya vitanda majumbani mfumo ambao haukuwa salama.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo kwa vikundi vya wajasiliamali wanaowezeshwa na taasisi ya Care nchini, Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo wa Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela alisema akaunti hiyo itawasaidia wajasiliamali hao pamoja na vikundi vingine mbalimbali ambavyo vilikuwa vikikusanya fedha zao na kuhifadhi kwa mwanakikundi majumbani kitendo ambacho si salama.
"..Hivyo NMB kwa kushirikiana na Care imeamua kuja na bidhaa ambayo itawasaidia wanakikundi hawa na wananchi wa Tanzania kwa ujumla, Ankaunti ambayo tunaianzisha inaitwa 'NMB Pamoja Account' ambayo inawawezesha wanakikundi kutunza fedha zao kwa pamoja huku zikiwa salama na kuongezeka riba," alisema Abdulmajid Nsekela.
Alisema, NMB ili kurahisisha huduma hiyo inamawakala wengi maeneo mbalimbali nchini wanaotoa huduma kwa wateja wao ya kuweka na kuchukua fedha zao muda wowote na kupitia matawi yao yalioko maeneo mbalimbali nchini. Aliongeza kuwa bidhaa hiyo ambayo wameianzisha pia ni mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za kibenki za uhakika zinazo muwezesha kutunza amana zake sehemu ya uhakika na salama.
Alibainisha kuwa bidhaa hiyo tayari imeanza kwa majaribio katika mikoa mitatu ambayo ni Morogoro, Zanzibar na Pemba ambapo tayari vikundi miatatu ambavyo tayari vimeunganishwa katika bidhaa mpya ya 'NMB Pamoja Account'
Alisema akaunti hiyo itawasaidia zaidi wajasiliamali kwenye vikundi kwani NMB ni benki kubwa yenye mtandao upana ambao unamatawi takribani wilaya zote za Tanzania. "...Na kwa kushirikiana na Care sasa hivi tunaamini tutaweza kuwafikia wajasiliamali wengi kwenye vikundi ambao wamekuwa wakiwezeshwa kukabiliana na changamoto za maisha pamoja na kupatiwa elimu ya utunzaji fedha," alisema Abdulmajid Nsekela.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker aliupongeza uongozi wa Care kwa kukubali kuwaunganisha wajasiliamali kwenye vikundi vyao na kuweza kutumia huduma za kibenki kupitia bidhaa hiyo mpya, ambayo pamoja na mambo mengine itawafanya wanavikundi pia kunufaika na fursa zingine za kibenki ikiwemo mikopo katika vikundi hivyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kiufundi wa Shirika la Care, Oliva Kinabo alisema zaidi ya vikundi 20,000 vyenye takribani wanachama laki nne vimeanzishwa na kuwezeshwa na Shirika la Care maeneo mbalimbali nchini Tanzania ili kukabiliana na changamoto anuai za kiuchumi kwenye ngazi za familia.
No comments:
Post a Comment