(Picha na Benedict Liwenga-Maelezo)
Na Lilian Lundo
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Angellah Kairuki amemsimamisha kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma
Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake
Mhe.
Kairuki ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari katika moja ya kumbi zilizopo katika
ofisi za Utumishi wa Umma.
“Namsimamisha
Bwana Said Nassoro aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia
watumishi walioko chini yake na
kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo hususani katika matawi
yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,” alisema Mhe. Kairuki.
Mhe.
Kairuki aliongeza kwa kusema kuwa usimamizi
wa Bw. Nassoro ambao haukuwa wa ufanisi
umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za Umma
ambapo mwaka 2011 na 2013 aliyekuwa
mkurugenzi wa chuo upande wa tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za
ujenzi.
Aidha
taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU zilithibitisha
ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza kuchukua hatua yoyote badala
yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye tawi la Tabora na kuendelea na
wadhifa wake.
Kutokana
na ubadhilifu huo imempelekea Mhe. Kairuki
kumsimamisha kazi Bw. Ngata ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Joseph Mbwiro kutokana na matumizi
mabaya ya fedha za malipo ya ada kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo
zilikuwa zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Mhe.
Kairuki ameendelea kueleza kuwa bado
wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao hawafuati mifumo
na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza watumishi ambao wanaonyeshe taswira nzuri na
kufuata mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma kwa ukamilifu wake.
No comments:
Post a Comment