Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumzia vipaumbele vya Serikali wakati wa mkutano na Wabunge kutoka nchini Sweden leo jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi nchini.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI
WA FEDHA NA MIPANGO AKUTANA NA WABUNGEWA SWEDEN
Waziriwa Fedha na
Mipango,Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na Wabunge wa Sweden katika ukumbi wa
Wizara hiyo, kuzungumzia ushirikiano baina Tanzania na Sweden.
Katika mazungumzo yake
na wabunge hao ambao wamewasili nchini kwa
ziara ya kikazi, Dkt. Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo makini
na inafanyakazi kwa ufanisi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma stahiki
kutokana na rasilimali zilizopo nchini.
Amesema Serikali imejipanga
kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ili kuiwezesha nchi kujiendesha yenyewe
na kuacha kutegemea misaada ya wahisani.
Aidha, amefafanua kuwa Tanzania
imejipanga kuongeza vyanzo vya ukusanyaji mapato pamoja na kuboresha vyanzo vilivyopo na kuhakikishakila Mwananchi
anayestahilikulipakodistahikianalipa kwa wakati.
“Ni aibu kwa nchi yenye
rasilimali za kutosha Wananchi wake kuishi katika hali ya umasikini, tunachotakiwa
ni kuboresha kilimo kwa sababu wananchi wengi ndicho wanachotegemea”, alisema.
Akizungumzia vipaumbele
vya Serikali katika mkutano huo, Dkt. Mpango alisema mkazo umewekwa zaidi katika
kufanya mapinduzi ya viwanda, ambapo nchi inaanzakuboresha viwanda vilivyopo hususani
vile ambavyo hutumia rasilimali zinazopatikana nchini kama zile zinazotokana na
kilimo.
Aliongeza kuwa katika kuboresha
viwanda pia Serikali ipo katika hatua za kuboresha soko la ndani na nje ya nchi
kwa bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo.
Dkt. Mpango alisema sambamba
na kufanya mapinduzi ya viwanda, Tanzania imejipanga kuboresha miundombinu ambapo
mpaka sasa kuna miradi mbalimbali ya maendeleo imeanzishwa kama mradi wa umeme vijijini.
Alisema katika suala la
umeme, nchi imeazimia kujikita katika uzalishaji wa kutumia vyanzo vingine kama
gesi asilia, jua na upepo kuliko kutegemea maji pekee.
Kuhusu sekta ya usafirishaji,
Dkt. Mpango amesema Serikali imejipanga kuboresha bandari zote nchini na kuzifanya
ziwe za kisasa ili kuhamasisha biashara za ndani na nje ya nchi kupitia bandari
hizo.
Hata hivyo, Dkt. Mpango
alikiri kuwa uboreshaji wa reli ya kati ni changamoto kwani reli hiyo haiwezi kuboreshwa
kwa kutumia fedha za bajeti ya Serikali pekee, hivyo Serikali inajitahidi kutafuta
njia za kufanikisha ujenzi huo.
Katika mkutano huo,
Dkt. Mpango alizungumzia suala la huduma za kijamii alisema, nchi imejipanga kutoa
elimu inayoendana na soko la ajira na Serikali imeanza kutoa elimu ya msingi na
sekondari bila malipo ili kuwawezesha wananchi wengi kupata elimu.
Akizungumzia suala la
uchumi, Dkt. Mpango alisema hali ya uchumi kwa sasa ni nzuri kwani pato la
ndani la Taifa limefika asilimia 7 katika miaka ya hivi karibuni.
Dkt. Mpango alisema ili
kufanikisha vipaumbele hivyo, ni lazima maadili na nidhamu ya kazi vifuatwe na
watendaji pamoja na watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aliongeza kuwa Serikali
ipo msatari wa mbele kupambana na rushwa na haitosita kuhakikisha watu wote wanaohusika
na rushwa wanachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande Wabunge kutoka nchini Sweden, wakiongozwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Kenneth Forslund, wameipongeza Serikali
ya Awamu ya Tano kwa jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutoa huduma za kijamii.
Tanzania na Swede nzime
kuwa na ushirikiano wa muda mrefu ambao umeifaidisha Tanzania katika shughuli mbalimbali
za maendeleo ikiwemo kuendeleza miradi ya afya na umeme hususani vijijini, elimu
pamoja na kusaidia kukamilisha bajeti ya kila mwaka.
Imetollewa
na Msemaji
Wizara
ya Fedhana Mipango
Kitengo
cha Habari
19.2.2016
No comments:
Post a Comment