Na
Nyakongo Manyama
MAELEZO
Dar
es Salaam
23.02.2016
HALMASHAURI Wilaya ya Kinondoni
Jijini Dar es Salaam katika mwaka kipindi cha 2016/17 imepanga kununua magari
40 yatakayotumika kwa ajili ya zoezi la ukusanyaji wa taka ngumu katika Kata na
Mitaa ya Halmashauri hiyo.
Hatua inaelezwa itasaidia
kuondoa kero ya mlindukano wa taka ngumu ambazo huzagaa ovyo, kutokana na
hushindwa kukusanywa kwa wakati na makampuni ya wakandarasi wa usafi katika
Kata na Mitaa wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza na MAELEZO
leo (Jumanne Februari 23, 2016), Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Sebastian
Mhowera alisema tayari ofisi hiyo pamoja na Halmashauri za Wilaya ya Ilala na
Temeke zimewasilisha ombi maalum la kuomba kibali cha ununuzi wa magari hayo
katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Kwa mujibu wa Mhowera
alisema Halmashauri hiyo huzalisha jumla tani 2020 za taka ngumu ambapo uwezo
uliopo ni kuteketeza tani 1300 kwa siku, na hivyo kiasi kinachobaki huibua
changamoto katika namna ya kukabiliana na ongezeko hilo.
“Kiasi kikubwa cha taka
zinazozalishwa nyingi hubakia mitaani na hazifiki barabarani ambapo ndipo
hukusanywa kwa ajili ya kupelekwa dampo, kwani vitendea kazi katika maeneo hayo
ni changamoto” alisema Mhowera.
Alisema kwa mujibu wa
Sera ya Usafi, Makampuni ya Wakandarasi wa Usafi yaliyopo katika Mitaa yana
wajibu wa kukusanya taka zote kwani husimamiwa na wananchi wenyewe, ambapo hata
hivyo makandarasi mengi yamekuwa hayana uwezo wa kufanya kazi hiyo.
Aidha Mhowera alisema
katika kufanikisha zoezi la usafi wa mazingira linalofanyika kila mwisho wa
mwezi nchini, Halamshauri hiyo imetoa maelezo mbalimbali ya kiutendaji kwa
Maaafisa Watendaji wa Mitaa na Kata.
No comments:
Post a Comment