Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw.
Dionis Malinzi wa pili kutoka kushoto akiongea na wanahabari (hawapo pichani)
kuhusu uteuzi wa ndugu Said Kiganja kuwa Kaimu Katibu Mtendaji mpya wa Baraza
hilo, wa kwanza kulia ni Msemaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bi. Zawadi Msala na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Rasilimali watu. (Picha na Benjamin
Sawe-WHUSM)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BMT
IMEMTEUA BWANA MOHAMED KIGANJA KUWA KATIBU MTENDAJI MPYA.
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limemteua
Bwana Said Kiganja kuwa Katibu Mtendaji
mpya wa Baraza hilo kuanzia leo, ili kujanza nafasi ya aliyekuwa Katibu
Mtendaji Baraza hilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye na kumrudisha Wizarani ili aweze
kupangiwa majukumu mengine.
Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria
iliyoundwa na BMT kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT
kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.
Kabla ya uteuzi huo Bwana Kiganja alikuwa ni Afisa Michezo Mkuu katika
ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka
2015 mpaka uteuzi wake ulipo fanyika.
Pia bwana Kiganja aliwahi kufanya kazi
kama Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo
Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
Bwana Kiganja ana shahada ya kwanza ya elimu upande wa masuala ya
michezo na utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Imetolewa
na Mwenyekiti wa BMT
Deonis
Mallinzi
19/02/2016
No comments:
Post a Comment