Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Maafisa
Wandamizi wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Jeshi
hilo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Katika
hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya
kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati
mipya ya kupambana na uhalifu nchini. Watatu kulia meza kuu ni Inspekta
Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake kwa Maafisa
Waandamizi wa Jeshi lake, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (kulia) kuzungumza na maafisa hao kutoka mikoa yote
nchini na kuufungua Mkutano wao wa Mwaka unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake,
Waziri Kitwanga kabla ya kufungua mkutano huo, aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana
na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na
uhalifu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimshukuru Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya NMB nchini, Ineke Bussemaker, mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia), Shilingi Milioni 75 kwa ajili
ya kuudhamini Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka
Mikoa yote nchini. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Kitwanga katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, na aliwataka
Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na
pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.
Sehemu
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, wakimsikiliza mgeni rasmi,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na
maafisa hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,
Dar es Salaam kabla ya waziri huyo kuufungua Mkutano huo wa Mwaka wao wa Mwaka
kwa ajili ya kufanya tathimini ya utendaji wao pamoja na kuliboresha zaidi
Jeshi hilo. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka
Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya
Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiyajibu maswali
mbalimbali ya waandishi wa habari ambao walitaka kupata ufafanuzi zaidi kutokana
na hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi
la Polisi, unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius
Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kufanya
kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati
mipya ya kupambana na uhalifu nchini. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
******************************************************************************
No comments:
Post a Comment