Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimfafanulia jambo Mwekezaji
kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya
Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) na Rais wa Klabu
ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), wakati wawekezaji
hao walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa
ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya
Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa TPSF ambaye
pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimsikiliza Mwekezaji
kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya
Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) wakati alipokuwa
akitoa ufafanuzi wa majukumu mbalimbali wanayoyafanya katika kampuni yake. Kulia kwake ni Rais wa Klabu ya
Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl. Wawekezaji hao walipomtembelea Waziri
Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala
mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio
wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na
Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na wawekezaji kutoka Bara la Ulaya, ambao ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje
wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia),
Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), Kushoto
ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya
Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc)-(ESSB), Dk. Alawi Swabury, na
wapili kushoto ni Mwakilishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambaye
pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. Wawekezaji
hao walikutana katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment