Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 6 September 2015

UVCCM YASEMA, CHADEMA ISITAFUTE MCHAWI, IMEJILOGA YENYEWE

NA BEATRICE SHAYO
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kisihangaike kutafuta mchawi kwani kimejiloga chenyewe kupitia migogoro yao inayoendelea.
 
Aidha, UVCCM umesema kuwa Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, hakupewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha urais kwa kuwa alikuwa na misingi mibovu ndani ya chama.
 
Katibu wa Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano Egla Mamoto, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tathimini ya kampeni ya uchaguzi inavyoendelea nchini.
 
Alisema CCM kwa sasa imejikita kutafuta kura na hakina muda wa kulumbana na Chadema na kukitaka kisitafute mchawi kwa kuwa wameshajivuruga wenyewe.
 
Alisema migogoro yao inaikuza CCM kimtaji na wataendelea kushikilia dola ili amani iendelee kutawala nchini.
 
Alisema watu waliokataliwa na CCM baada ya kubainika wana mifumo mibovu Ukawa umewapokea hivyo UVCCM itaendelea kuelimisha umma kutambua kiongozi bora.
 
Akizungumzia tathimini ya kampeni ya uchaguzi zinavyoendelea alisema kuwa tafiti inaonyesha kuwa CCM inakubalika kwa asilimia 78 baada ya mgombea wao wa urais Dk. John Magufuli kufanya ziara katika mikoa mbalimbali. 
 
Alisema CCM imezidi kukubalika na kufikia asilimia 85.
 
Alisema ongezeko hilo limechangiwa na rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi uliotukuka wa mgombea wao pamoja na uwezo mkubwa aliouonyesha katika kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi.
 
Ukimuangalia Dk. Magufuli unaona kabisa anachokitamka kinaendana na mwonekano wake, kwa mfano anaposema nachukia rushwa na ufisadi ataunda mahakama ya kushughulikia wezi na mafisadi hata wengine wakijaribu kukemea ufisadi unaona kabisa wanachokisema hawamaanishi na hawana nguvu ya kutamka maneno hayo, alisema Mamoto.
 
Alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imetoa ratiba kila mgombea anatakiwa kuwafikia wananchi ili akanadi sera za chama chake lakini baadhi ya wagombea wameanza kuonyesha dalili za kuchoka na kushindwa kufika katika maeneo mengine.
 
Mamoto alisema kitendo cha kutowafikia wananchi wengine ni dalili za kuwabagua watanzania. 
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment