
Na Hastin Liumba, Sikonge
SERIKALI wilaya ya Sikonge
mkoani Tabora imesema itaendelea kuboresha na kuongeza thamani ya zao la Nyuki
sanjari na kuagiza kila kaya kuwa na mizinga miwili ya Nyuki ili kuweza
kujiongezea kipato.
Mkuu wa wilaya ya Sikonge
Hanifa Selengu alisema hayo kwenye mafunzo kwa wajasiliamali wanaushirika
wanaofuga Nyuki, mafunzo ambayo yaliendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la
TRADE CRAFT toka nchini Uingereza.
Selengu alisema serikali
imeweka jitihada zake kuhakikisha sekta ya Nyuki wilayani Sikonge inafanikiwa
na sasa imeanzisha Mashamba darasa sanjari na kuyasimamia kwa ukaribu.
Hata hivyo aliwaomba
washiriki wamafunzo hayo kutumia elimu, fursa na mafunzo watakayopata ili
waondokane na umasikini wao wa kutumia sekta ya ufugaji Nyuki kupata kipato.
Mkuu huyo wa wilaya
alisema hadi sasa Sikonge imezalisha asali tani 287 hadi kufikia mwaka 2014
lakini akawataka wafugaji hao kuendelea kujiunga kwenye vyama vya Ushirika.
Alisema hadi kupindi hiki
zinahitajika tani 20 za asali ambazo ni sawa na Ndoo 600 za ya asali na hadi
sasa jumla ya Ndoo 400 zimeshapatikana.
Kwa upande wake Afisa
Mwezeshaji wa shirika la TRADE CRFT ‘Beet Project’ Job Chimwaga alisema
hadi sasa katika wilaya ya Sikonge katika mafunzo hayo wamefikiwa wafugaji
Nyuki 300 wakiwemo wanawake 121 na wanaume ni 179.
Alisema wilaya hiyo hadi
sasa ina jumla ya wafugaji Nyuki wapatao 2,160 ambao wanatambulika na aliwataka
kutumia mafunzo wapatayo kuzalisha asali bora na kuepuka uchakachuaji.
No comments:
Post a Comment