Na Hastin Liumba, Tabora
MAMLAKA ya Mapato Tanzania
(TRA) mkoa wa Tabora imevuka lengo la makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha wa
2013/2014 na kufanikiwa kukusanya sh Bilioni 15.47 sawa na asilimia 102.
Meneja wa mamlaka ya
mapato (TRA) mkoa wa Tabora Paulo Werema Laurant alisema hayo wakati akifanya
mahojiano na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mkoani hapa.
Laurant alisema katika
mwaka wa fedha wa 2013/2014 mkoa uliweka lengo la kukusanya sh Bilioni 15.14 na
walifanikiwa kukusanya sh Bilioni 15.47 sawa na asilimia 102.
Alisema TRA kupitia
mkakati wake wa nne wa miaka mitano 2013/2014-2017/18 ambao upo katika mwaka wa
pili wa utekelezaji wake una lengo la kuongeza pato la taifa kwa asilimia 19.9
kufikia mwaka 2017/2018 ikiwa ni sehemu ya azma ya kuongeza mapato ya ndani na kupunguza
sehemu ya utegemezi.
Laurant alibainisa kwa
mwaka wa fedha wa 2014/2015 mkoa umepewa jukumu la kukusanya kiasi
cha sh Bilioni 19.36 ikiwa ni ongezeko la asilimia 22 ya lengo la mwaka wa
fedha wa 2013/2014 na hiyo ni moja ya changamoto kwa mkoa kwani kuna vyanzo
vichache vya mapato.
Alitaja changamoto
nyingine ni suala la elimu bado ni changamoto kwa walipa kodi hivyo kupelekea
biashara nyingi kukosa kumbukumbu nzuri.
Aidha nyingine ni mwitikio
mdogo kwa raia kutoa taarifa za wakwepa kodi,mwitikio mdogo katika ununuzi wa
mashine za kutolea risiti (EFDs) awamu ya pili ikiwa lengo ni kusajili
wafanyabiashara 3,716 kufikia mwezi Disemba 31,2013 kwani ni wafanyabiashara 69
tu sawa na asilimia 1.86 ndiyo wamenunua mashine hizi.
Hata hivyo alisema wamejipanga
kukabiliana na changamoto hizo ikiwa ni kuendelea kutoa elimu,kufuatilia kwa
ukaribu matumizi ya mashine na kupanua wigo wa kodi kwa kusajili biashara zote
zinazostahili.
No comments:
Post a Comment