
Hii ni taswira ya vyoo vingi vya vijijini na hata katika miji midogo nchini
Na HastinLiumba, Sikonge
WAKAZI wa wilaya ya
Sikonge mkoa wa Tabora wameagizwa kila kaya kuwana vyoo bora ili kujilinda na
magonjwa yatokanayo na uchafu.
Mkuu wa wilaya ya
Sikonge Hanifa Selengu alisema hayo kwenye kilelecha siku ya Mazingira duniani
ambacho kilifanyika katika kata ya Molewilayani humo.
Selengu alisema hali
ni mbaya katika baadhi ya kaya kwani inaonyeshawakazi hao wanajisadia vichakani
kwani ni asilimia 70 ya magonjwayanatokana na uchafu na hivyo ni vyema wananchi
sasa wakabadilika nakuwa na vyoo bora.
Alisema magonjwa kama
Ebola,kuharisha na homa za matumbo zinatokana nauchafu hivyo ni vyema wananchi
wakabadilika na kuachana na tabia zakuwa na imani potofu.
“Ni kaya 89 katika
kijiji cha Usanganya hapa tunapoadhimisha siku hiii...bado ni asilimia ndogo
zenye vyoo kulinganisha na wakazi wakata hiyo hii n hatari iliyo mbeleni kwetu
tujenge vyoo sasa,”alisema
Selengu.
Selengu.
Kaimu afisa afya wa
wilaya ya Sikonge Laurent Lushekya katika taarifayake alisema hadi mwaka 2013
kaya ambazo hazina vyoo zimepunguakutoka asilimia 15.5 mwaka huo hadi
asilimia 13.8.
Alisema kaya zenye
vyoo bora zimeongezeka kutoka asilimia 10.5 mwaka2013 hadi asilimia 25.8 kwa
mwaka 2014.
Alisema wilaya imepewa
malengo ya kitaifa ya kuwa na vyoo bora 1,458ifikapo mwaka 2016 na kutakiwa
kufikia asilimia 50 ambapo ni vyoo 729ifikapo Desemba mwaka 2014.
Lushekya aliongeza
takwimu zilizopo zinaonyesha wilaya imefikiaasilimia 53 kuwa na vyoo bora 778
katika vijiji vilivyo katika kampeniya susafi wa mazingira.
Hata hivyo alisema
wamejipanga kuhamasisha vijiji vyote vya wilaya yaSikonge kuhusiana na afya ya
usafi na mazingira.
No comments:
Post a Comment