Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 8 September 2016

WAZIRI ASEMA, NI KINYUME CHA SHERIA KWA MGAMBO KUWANYANYASA WAFANYABIASHARA WADOGO.

Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jaffo 

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, Dodoma
08/09/2016
Serikali imesema ni kinyume cha sheria kwa askari mgambo kuwanyanyasa Mama Lishe na wafanyabiashara wengine wadogo nchini.

Akijibu swali la Mhe. Zaynab Vulu (Viti Maalumu) alilotaka kujua kwanini Serikali isiandae mazingira mazuri ya kufanyia kazi wafanyabiashara hao, Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jaffo amemesema kuwa askari mgambo wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu bila kuwanyanyasa wala kuwadhulumu wakati wakiwaondoa katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Naibu Waziri Jaffo aongeza kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wafanyabiashara hao walioko katika sekta isiyo rasmi katika kukuza kipato na ajira.

Aidha, Naibu Waziri Jaffo amesema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa askari mgambo yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya kuwanyanyasa wafanyabiashara na Mama Lishe wanapotekeleza majukumu yao.

Mbali na hayo, Naibu Waziri amezikumbusha  Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwemo Mama Lishe karibu na maeneo walipo wateja wao.

Zaidi ya hayo Naibu Waziri huyo amewataka wafanyabiashara wadogo nchini kufanya biashara katika maeneo yaliyotengwa rasmi na Halmashauri na kuacha kufanya biashara hizo katika maeneo yasiyoruhusiwa.

No comments:

Post a Comment