Ofisi ya Makamu wa
Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba
kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli
wowote.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA
TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Anuani ya Simu: “MAKAMU” Ofisi ya Makamu wa Rais,
Simu Na.: 2116919
6 Barabara ya Albert Luthuli,
Fax Na: 2116990 S.L.P. 5380,
Unapojibu taja: 11406 Dar es Salaam,
6 Septemba, 2016
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: KUKANUSHA
TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE
MITANDAO MBALIMBALI YA
KIJAMII
Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye
mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya
uzushi na uongo haina ukweli wowote.
Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye
taharuki. Mhe. Makamu wa Rais yuko bega
kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi
zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla
kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri
uliopo baina ya Viongozi wetu.
Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa
bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment