Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Friday 4 September 2015
WANANCHI WATOA ARIDHI EKARI 42 ZA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA
Na Hastin Liumba, TaboraWANANCHI wa kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora waliokuwa na mgogoro wa ardhi dhidi ya Halmashauri ya manispaa ya Tabora katika eneo la Uledi wametoa Hekari (40) za Ardhi yao na kuikabidhi serikali kwa ajiri ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Tabora Mjini.
Hatua hiyo imefuatia baada ya maridhiano kufanyika dhidi ya pande hizo mbili zilizokuwa na mgogoro wa aridhi uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano bila kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.
Wakizungumza kwanyakati tofauti katika zoezi la upimaji hekari hizo walisema malumbano hayo hayana umuhimu na kuona kutoa hekari hizo ili waweze kunufaika na huduma bora ya afya itakayo hudumia wananchi wengi zaidi.
Amani Mbwambo Mkazi wa Tabora manispaa alisema kwa sasa mgogoro huo umekwisha na kuwataka wananchi kuunga mkono maridhiano hayo iliwaweze kupata maendeleo haraka.
Azizi Kitamanwa mkazi wa Ipuli uledi Tabora manispaa alisema serikali inapaswa kuwa inatatua haraka migogoro ya aridhi ili wananchi waweze kuendelea na maendeleo ya kijamii.
Afisa Mipango miji manispaa ya Tabora Godard Mwakalukwa alisema ili migogoro ya aridhi iweze kupungua suala la ushirikishwaji wananchi lizingatiwe na kupewa uzito na viongozi wa serikali.
Ofisa huyo aliwapongeza wananchi hao kwa kufikia maamuzi hayo ya kukata hekari 40 na kuikabidhi serikali dhidi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya kuwa ni jambo la kujivunia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ardhi Plan Limited Gombo Samandito alisema tayari Kampuni yake kwa kushirikiana na Wananchi wa eneo hilo la Uledi imekwishapima viwanja zaidi ya elfu nane kwa ajili ya makazi ya Wananchi huku ikitenga maeneo ya huduma za kijamii kama Shule,Soko na maeneo
ya wazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment