Afisa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gordon
Nsajigwa akimpatia mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya
wanawake tiketi jana jioni tayari kwa
safari ya kuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African
Games), kushoto aliyevaa suti ni Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo. (Picha
na Benjamin Sawe- WHVUM).
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda
ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) jana jioni tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini
Congo Brazaville kwa ajili ya Mashindano ya Afrika (All African Games). (Picha na Benjamin Sawe- WHVUM).
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.
Leonard Thadeo kushoto akimkabidhi mmoja wa wanariadha Bendera ya Taifa tayari
kwa safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All
African Games), Timu hiyo iliondoka jana jioni na ndege ya Shirika la Ndege la
Tanzania. (Picha na Benjamin Sawe-
WHVUM).
No comments:
Post a Comment