Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 9 September 2015

MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA KUPATIKANA KESHO

Rais Jakaya Kikwete na Kaimu Mufti wa Tanzania,
Rais Jakaya Kikwete na Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir. 

Na Rachel Chibwete
Dodoma. Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, anatarajiwa kupatikana kesho katika mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), utakaofanyika mjini hapa.

Akizungumza jana, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shaaban alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na wajumbe wameanza kuwasili.

Sheikh Shaaban alisema hadi sasa, kuna masheikh wanne, wanaowania wadhifa huo wa juu katika dini ya Kiislamu Tanzania.

Aliwataja wagombea hao ni pamoja na Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir, Sheikh Ally Mkoyogole, Sheikh Hamis Mtupa na Sheikh Hassan Kibulwa.

Sheikh Shaaban aliwataja wajumbe wa mkutamo huo kuwa ni masheikh wote wa mikoa na wilaya ambao wanaunda Tume ya Dini, wenyeviti wote wa halmashauri za mikoa pamoja na makatibu wao, na wenyeviti wote wa wilaya nchini pamoja na makatibu wao.

Aliwataja wajumbe wengine kuwa ni wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Baraza la Ulamaa na wajumbe wa Halmashauri Kuu.

“Natoa wito kwa Waislamu nchini kusubiri kwani Mungu ndiye anayeweza kumjua kiongozi ni nani,” alisema Sheikh Shaaban.

Uchaguzi huu wa Mufti unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa bin Shaaban Simba kilichotokea Juni 15. Simba alikuwa Mufti wa pili tangu kuanzishwa kwa Bakwata, akitanguliwa na Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed ambaye naye ni marehemu.

CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment