Meneja wa
Bia chapa ya Serengeti, Rugambo Rodney katikati
akithibitisha namba ya simu ya mkononi
ya mshindi wa Limo Bajaj, wakati wa kuchezesha droo hiyo ya “tutoke na Serengeti” (kulia) ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed, na kushoto ni Mkaguzi kutoka
Pricewatercoopers, Golder Kamuzora. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya
Serengeti jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi toka
Pricewatercoopers, Golder Kamuzora akithibitisha namba ya mshindi wa Limo
bajaji, wakati wa kuchezesha droo ya kumtafuta mshindi wa pili wa limo bajaj,
katikati ni Meneja wa Bia chapa ya Serengeti, Rugambo Rodney na kulia ni
Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed. Hafla hiyo ilifanyika Serengeti mjini Dar es Salaam.
Meneja wa bia
chapa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney , akiongea kwa simu na mshindi wa Limo
bajaj ya Pili kutolewa katika shindano la “Tutoke na Serengeti” Peter Emanuel
mkazi wa Rombo Kilimanjaro katika shindano linaloendeshwa na ka mpuni hiyo ya
bia ya Serengeti. Kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed. Hafla hiyo ilifanyika
Serengeti mjini Dar es Salaam.
Meneja wa
bia chapa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney , akifafanua jambo wakati wa
kuchezesha shindano la” Tutoke na Serengeti” ambapo Peter Emanuel mkazi wa
Rombo mkoani nkilimanjaro ameibuka mshindin kwa kujinyakulia Limo Bajaj yenye
thamani ya Sh. 7 milioni. Kulia ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdullah Hemed.
Meneja wa
bia chapa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney, katikati akifafanua jambo wakati wa
kuchezesha shindano la” Tutoke na Serengeti” ambapo Peter Emanuel mkazi wa
Rombo mkoani nkilimanjaro ameibuka mshindin kwa kujinyakulia Limo Bajaj yenye
thamani ya Sh. 7 milioni. Kulia ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdullah Hemed na kushoto
ni Mkaguzi toka Pricewatercoopers, Golder Kamuzora. Hafla hiyo ilifanyika makao
makuu ya Serengeti, jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Rombo Bwana Peter Emmanuel mwenye miaka 37
ameibuka mshindi wa pili wa Limo Bajaj katika droo ya pili ya kampeni ya miezi
mitatu ijulikanayo kama “Tutoke na Serengeti”, inayodhaminiwa na Serengeti
Breweries Ltd ikishirikiana na B-Pesa.
“Ninafuraha sana pia namshukuru Mungu...hii ni siku
nzuri sana kwangu. Asante Serengeti kwa zawadi hii na ninaahidi kuendelea
kushiriki katika promosheni hii, hata ikiwezekana kushinda bajaji nyingine.”
Alisema Bajaj hiyo itamuongezea kipato kwa zaidi ya asilimia 30. Mara tu baada
ya kutaarifiwa kwa njia ya simu kwamba amejishindia Limo Bajaj. Sambamba na hilo
Bi Valerian Moshi mkulima wa Moshi vijijini ni mshindi mwingine aliyejipatia
Tsh. 100,000/=
Kampeni hii ya nchi nzima ilizinduliwa rasmi na
kampuni ya SBL pamoja na B-Pesa mwanzoni mwa mwezi uliopita na imekuwa
ikiwazawadia wateja wake kila wiki katika kila
droo iliyokuwa ikifanywa na SBL chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya
bahati nasibu Tanzania.
Baadhi ya washindi waliofaidika na kupata
zawadi katika kampeni hii ni pamoja
na : -Bi. Rukia Almasi ambaye ni mama wa
nyumbani na mkazi wa Kihonda aliyejishindia Limo Bajaj ya kwanza na Hassan Mfaume aliyeshinda
safari ya siku mbili kutembelea Serengeti National park ambayo itaigharimu SBL takriban Tsh 10 milioni.
Akizungumza na vyombo vya habari, Bwana. Rugambo
Rodney-Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager alisema, “kadiri kampeni
inavyoendelea, watu wengi wataendelea kushinda zawadi mbalimbali. Zaidi ya
bajaji, zawadi nyingine ni pamoja na:- safari ya bure kwa wapenzi kutembelea
hifadhi za taifa, fedha taslim za papo kwa papo za thamani ya shilingi 5,000/=
, punguzo la shilingi 300/= katika gharama halisi ya bia pamoja na bia za bure
zinazopatikana katika baa zote nchi nzima”.
Rodney aliendelea kusema kwamba, kwa miaka mingi sasa,
Serengeti imekuwa ikiamini katika kurudisha kiasi cha faida kwa jamiii kupitia
kampeni mbalimbali ambapo Tutoke na Serengeti imelenga katika hilo”.
Ujumbe toka kwa Meneja Masoko wa kampuni ya B-Pesa Mwana. Salil Abbas ulisema kuwa bado
zipo Limo Bajaj 5 za kushindaniwa na kuwashauri watanzania kuendelaea kushiriki
katika kampeni .Kwenye promosheni hii, B-Pesa inahusika na usambazaji wa fedha
kwa washindi kwa njia ya simu za mkononi.
Ili kushiriki katika kampeni, mteja anatakiwa awe
na umri wa zaidi ya miaka 18. Kuingia katika droo na kushinda zawadi mbalimbali
mshiriki anatakiwa anunue bia ya Serengeti Premium Lager na kutuma number
atakazozikuta chini ya kizibo kwa ujumbe mfupi wa maneno kwenda number 15317. Kadiri utumavyo number zilizo katika
kizibo ndivyo unavyojiweka katika nafasi ya kushinda.
No comments:
Post a Comment