Baadhi ya wanawarsha kutoka Malawi na Tanzania wakati wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.
Dkt. Agnes Kijazi akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.
Mkufunzi wa warsha kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa Uingereza bw. David Hein akiendesha mafunzo kwa wanawarsha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
WARSHA
YA KISAYANSI KUHUSU HUDUMA ZA HALI YA HEWA KUPITIA MODELI YA ‘PRECIS’, KUANZIA TAREHE 29 JUNI HADI 3 JULAI 2015, DAR
ES SALAAM, TANZANIA.
Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
wameandaa mafunzo ya hali ya hewa kwa
kutumia modeli ya PRECIS (Providing
Regional Climates for Impact Studies) kuanzia
tarehe 29 Juni hadi 03 Julai 2015. Warsha/
mafunzo haya yameandaliwa na TMA chini ya mwamvuli wa mradi wa GFCS unaotekelezwa
kwa upande wa Afrika katika nchi za Tanzania na Malawi
Washiriki wa mafunzo hayo
kutoka TMA na Kurugenzi ya Hali ya Hewa ya Malawi wanategemea kujifunza matumizi ya modeli ya
PRECIS kutoka kwa mtaalamu kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambayo
imekuwa ikitumia modeli hiyo katika utekelezaji wa huduma za hali ya hewa.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni
kuongeza uelewa wa utoaji huduma za hali ya hewa pamoja na kuweza kutoa taarifa
sahihi za muda mrefu zenye kuweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya
hali ya hewa na tabia nchi. Alisema Dkt.Kijazi
PRECIS ni mfumo unaweza kutoa taarifa za hali
ya hewa za muda mrefu (Klimatolojia) kwa eneo husika.
Imetolewa na Monica Mutoni,
Afisa Uhisiano. TMA
No comments:
Post a Comment