Rais wa Marekani Barrack Obama amesifu uwezo wa biashara na uchumi wa bara Afrika kwenye hotuba yake ya kwanza tangu aingie nchini Kenya siku ya Ijumaa.
"Africa inasonga mbele,.. watu wanainuliwa kutoka kwa umasikini.
'' mapato yanapanda na idadi ya matajiri inaongezeka’’
Obama alisema hayo kwenye hotuba ya uzinduzi wa Kongamano la wajasiria mali.
Rais Obama alizuru kumbukumbu ya ubalozi wa Marekani uliolipuliwa na bomu mwaka wa 1998, kabla ya majadiliano ya usalama na rais wa Kenya katika ikulu ya Nairobi.
Obama ni rais wa kwanza wa Marekani kuzuru nchi ya Kenya.
Ziara hii imetajwa kama kurejea nyumbani na vyombo vya habari vya Kenya, huku mamia ya watu wakijitokeza kumshangilia rais huyo ambaye baba yake ni mzaliwa wa Kenya.
Shughuli ya kwanza ya Obama ilikuwa ni kuhutubia Kongamano la wajasiria mali kutoka mataifa 120 kote duniani.
Alisema Afrika yapasa kuwa chemchemi ya maendeleo ya siku za usoni, na kuongeza kuwa serikali zinafaa kuhakikisha kuwa ufisadi haukiti kambi.
Aidha Obama alinena kuwa Kenya imeendelea sana tangu awe nchini humo mara ya mwisho. ‘nilipokuwa hapa Nairobi miaka kumi iliyopita, ilikuwa tofauti sana na ilivyo sasa’.
Rais Obama hivi sasa yuko katika ikulu ya Nairobi anakotarajiwa kutia sahihi makubaliano ya kiuchumi baina ya taifa lake na Kenya.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment