Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama anaendelea na ziara yake nchini Ethiopia ambapo leo anatarajiwa kutoa hotuba kwa viongozi wa muungano wa Afrika.
Suala la usalama, demokrasia na utawala bora ni mada kuu alizozibeba katika ziara yake anayoifanya katika mataifa ya Afrika .
Jana jioni rais Obama alikutana na viongozi wa nchi za mashariki na pembe ya Afrika IGAD, kuzungumzia usalama hasa katika taifa changa zaidi duniani la Sudan kusini.
Obama atakuwa rais wa kwanza wa Marekani kutoa hotuba kwa wanachama 54 wa umoja huo ,huku swala la usalama na vita dhidi ya ugaidi ikiwa ni miongoni mwa ajenda zake kuu.
Siku ya jumatatu rais Obama aliipongeza Ethiopia kama mshirika mkuu katika kukabilana na magaidi.
Amesema kuwa Ethiopia imechangia pakubwa katika kudhoofisha uwezo wa kundi la kigaidi la Alshabaab nchini Somalia.
Rais huyo wa Marekani alikuwa akizungumza baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati wa ziara ya kwanza ya kiongozi wa Marekani katika taifa hilo la Afrika mashariki.
Pia alitoa wito kwa Hailemariam kuimarisha rekodi ya haki za binaadamu na utawala bora.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment