Juu ni picha zinazomuonyesha Zuwena Mohammed 'Shilole' akiwa katika matukio mbalimbali huku akiwa ameaacha maungo yake wazi.
National Arts Council BASATA
Tarehe:
31/07/2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BASATA Arts Centre
Tel. 2863748/2860485
Fax:
0255- (022) – 286 0486
Ilala
Sharif Shamba
P.O.
Box. 4779, Dar es Salaam
E-mail:basata06@yahoo.com
YAH: KUFUNGIWA KWA MSANII ZUENA
MOHAMED MAARUFU KAMA SHILOLE KUJISHUGHULISHA NA KAZI ZA SANAA KWA MUDA WA MWAKA
MMOJA
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini
limemfungia msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zuena Mohamed kwa jina la kisanii
Shilole kufanya shughuli za sanaa nchini kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe
24/07/2015 hadi tarehe 24/07/2016.
Itakumbukwa
kuwa mnamo tarehe 09/05/2015 akiwa katika onyesho lake la Muziki nchini
Ubelgiji alikiuka
maadili ya kazi ya sanaa mbele ya hadhira ya wapenda sanaa
za Tanzania na hivyo akadhalilisha utu wake na jamii ya Kitanzania
kimaadili. Pia itakumbukwa kwamba mnamo
mwezi Oktoba, 2013 BASATA ilimuonya na akakiri kwa kuomba msamaha kwa tabia
yake ya kucheza bila kuzingatia utu na maadili
awapo jukwaani.
BASATA
ilimpa nafasi ya kutoa maelezo yake kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chake cha
kudhalilisha maadili, utu na sanaa ya Tanzania lakini akakaidi kutoa maelezo. Hivyo basi BASATA imejiridhisha kwamba alikiuka
maadili ya kazi ya sanaa kwenye onesho
lake la huko Ubelgiji makusudi na amekiuka Sheria,
Kanuni na
Taratibu za uendeshaji wa Sanaa.
Hivyo
basi kutokana na ukiukwaji huo wa sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za
sanaa nchini, Baraza la Sanaa la Taifa chini ya Kanuni ya 30(1)(d) ya G.N 322 ya 2005 limemsimamisha kujishughulisha na
kazi za Sanaa nchini kwa muda wa Mwaka Mmoja tokea tarehe 24/07/2015.
Hivyo
haruhusiwi kufanya au kushiriki kwa namna yoyote ile shughuli yoyote ya onesho
la sanaa nchini au nje ya nchi. Iwapo atafanya kinyume cha hayo kutapelekea
kupewa adhabu zaidi ikiwa ni pamoja na yeyote yule utakaye shirikiana naye.
Ni matumaini ya Baraza la Sanaa la
Taifa kwamba wasanii na waandaaji wa shughuli za sanaa wataendelea kutambua
umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
Sanaa
ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
KATIBU
MTENDAJI
No comments:
Post a Comment