Kampuni ya magari ya Fiat Chrysler kutoka Marekani imeyarudisha magari yake yapatayo milioni 1.4 baada ya watafiti wa usalama kuonyesha kuwa magari yao yanaweza kudukuliwa.
Siku ya Jumanne gazeti la teknolojia Wired iliripoti kuwa wadukuzi wamechukua udhibiti wa gari la Jeep Cherokee kupitia mtandao wa mfumo wa burudani.
Chrysler imesema imetoa agizo hilo kwa wamiliki wa magari hayo waliojitolea kuyarudisha.
Kampuni hiyo imesema kuwa udukuzi wa magari yake ni uhalifu.
Watafiti wa usalama Charlie Miller na Chris Valasek walionyesha kuwa wadukuzi hao wanaweza kuyadhibiti magari ya Jeep Cherokee kwa kutumia rimoti, ukitumia mfumo wa burudani wa gari hilo ambalo unashirikiana na mtandao wa simu.
Watafiti hao wawili wa usalama wametumia miaka 5 kuchunguza mifumo ya magari na kubuni mipango ya kuikabili.
Wawili hao wanatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu kazi yao katika kongamano la Defcon hackers mwezi ujao.
Muda mfupi baada ya tangazo hilo kutolewa ,Bwana Miller aliandika katika akaunti yake ya twitter kuwa anashangazwa na ni kipi nafuu kati ya kutengeza magari salama ama kuyarudisha iwapo kuna tatizo.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment