Katika mchakato huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha ualimu Tabora mchakato ulihusisha wagombea watano na jumla kata 29 zilizoko manispaa Tabora zilishiriki.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Mwasubila Ntambo alisema Peter Mkufya alishinda kwa kupata kura 148 na kuibuka kidedea.
Alisema Profesa Nhomba alishika nafasi ya pili baada ya kupata kura 61,akifuatiwa na kura Said Mwasekela 51,Maganga Raymond Kura37 na Furaha Jafar Kura 20.
Peter Mkufya baada ya kuibuka kidedea alisema atahakikisha anafanya kila liwezekanalo kushinda jimbo la Tabora mjini kwani anaamini kwa sasa ipo haja ya kufanya mageuzi na kuandika historia ya Tabora kutoa mbunge toka CHADEMA.
Alisema kushinda inawezekana kwani mazingira ya ushindi yako wazi na akawaomba wanachama wenzake kumuunga mkono ili kuing`oa CCM jimbo la Tabora mjini.
Alisema wananchi wa jimbo hilo ni kama walikuwa yatima kwani huduma nyingi za kijamii zilikuwa ni duni na hazikupata mtu wa kuwasemea.
Mkufya ambaye ni mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya tumbaku ya TLTC Tabora alisema anaamini kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Tabora mjini atahakikisha wananchi wa Tabora wanapata huduma zinazostahiki.
Alisema anaamini historia ya Tabora mjini itabadilika hasa endapo atachaguliwa kwani atakuwa mwakilishi wa wananchi anayesimamia uwakilishi na uongozi wa kiutumishi (Servant Leadership).
Alisema kipaumbee chake cha kwanza ni elimu,huku akidai atatilia nguvu katika kusimamia Miundombinu ya barabara,Kilimo na afya.
No comments:
Post a Comment