Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi na Mbunge wa Jimbo la Igalula,Athumani Mfutakamba
>Dk Mfutakamba adaiwa kusambaza vipeperuhi vya kumchafua Musa ntimizi
Na Hastin Liumba, Uyui
MBUNGE wa jimbo la Igalula Dk Athuman Mfutakamba na mgombea mwenzake Musa Ntimizi almanusura wazichape kavukavu kufuatia Dk Mfutakamaba kusambaza vipeperushi vya kumkashifu mwenzake.
Vipeperushi hivyo ambavyo gazeti hili inavyo vinahusisha kesi ya Musa Ntimizi ambayoilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Joctan Rushwera na ilishafutwa na Mahakama Hakimu Mkazi wilaya ya Tabora kwa kukosa ushahidi.
Hatua hiyo ilifikiwa kutokana na Dk Mfutakamba kuendelea kuzomewa na wananchi na wanachama wa CCM katika baadhi ya maeneo wanapokuwa kwenye mikutano ya kujinadi.
Aidha kingine ni Dk Athuman Mfutakamba kudaiwa kugawa vipeperushi vinavyomkashifu Musa Ntimizi.
Hatua hiyo ndiyo iliyopelekea Musa Ntimizi kuhoji mgombea mwenzie ni vipi amekuwa akimdhalilisha kupitia vipeperushi hivyo.
Tukio la hilo lilijitokeza katika kata ya Tura wilaya ya Uyui baada ya wawili hao kutaka kuonyeshana umwamba muda mfupi kabla ya mkutano.
Kufuatia hali hiyo Dk Mfutakamba alionyesha kukerwa na hali hiyo akamvaa kwa maneno Musa Ntimizi akidai anawatuma wananchi wamuulize maswali makali na kumzomea.
Dk Mfutakamba alisikika akiwaambia watu kuwa Musa Ntimizi ndiye chanzo cha yeye kukumbwa na zomeazomea hiyo na maswali mazito.
Minong`ono hiyo ilimfanya Musa Ntimizi kumuuliza Dk Mfutakamba endapo anao ushahidi wa yeye kutuma wananchi na wanaCCM wamzomee kwani amechoshwa na maneno hayo ya kupandikiziwa.
“Mimi siwezi kuwatuma wananchi wamzomee yeye kwa lipi na mimi itanisadia nini nikifanya hayo…….kinachomponza mwenzangu na ananihisi mimi ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwani vipo vitu ambavyo aliwaahidi wananchi.”alisema Ntimizi.
Alisema kuna vitu ambavyo aliwaahidi wananchi sasa hajatekeleza hivyo wananchi wana haki ya kuuliza maswali kwani alikuwa mwakilishi wao kama mbunge wa jimbo la Igalula.
Ntimizi alisema alifikia hatua ya kuhoji ni vipi afikie hatu ya kuwaeleza watu mimi natuma wananchi wamzomee nashangaa mwenzangu anakuja juu na kutaka kupigana.
Ntimizi ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui alisema amechoshwa sana na kupakwa matope na kudhalilisha kiasi kikubwa hivyo anapenda kuona hali hiyo ya kuchafuliwa inakwisha.
Alisema anaandaa malalamiko kimaandishi na kuwasilisha kwa uongozi wa chama wilaya kwa hatua zaidi.
Alisema hapa kila mtu anawania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa oktoba hivyo tunapaswa kuwasikiliza wananchi na wanachama wetu wanapotuuliza maswa tusipaniki.
Dk Mfutakamba ambaye aliwahi kuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya Rais Dk Jakata Kikwete hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kwani alikuwa na jabza wakati huo hata alipotafutwa tena hakupatikana hata kwenye simu zake.
Jimbo la Igalula waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Dk Athuman Mfutakamba ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo, Musa Ntimizi na Hanifa Kitwana Kondo.
Katibu wa CCM wilaya ya Uyui Innocent Nanzabar alikiri kuwepo malalamiko toka kwa Musa Ntimizi juu ya vipeperushi hivyo ambavyo vipo kama ushahidi.
Alisema alilazimika kwenda eneo la tukio na baada ya kujiridhisha alikemea hali hiyo na kutoa mwongozo wa namna mchakato unavyoelekeza.
“Ni kweli nimekuta malalamiko na mzozo huo nimekemea hali hiyo kwamba wagombea kuchafuana vinginevyo tutachukua hatua kama chama endapo tutabaini na kuwa na ushahidi kama kuna mgombea alikiuka taratibu.’alisema Katibu huyo.
No comments:
Post a Comment