Bakari Mbelemba, maarufu Mzee Jangala
NA MWADISHI WETU
WASANII nchini wametakiwa
kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba katika mifuko mbalimbali ya jamii kwa kuwa
kufanya hivyo kuna kumuhimu mkubwa katika maisha yao baada kuwa wamestaafu kazi
zao au wanapokuwa hawana tena uwezo wa kufanya kazi.
Hayo yalisemwa na msanii
mkongwe wa maigizo hapa nchini Bakari Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala
wakati akizungumza katika Jukwaa la na Sanaa lililofanyika Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.
Mzee Jangala alikuwa
akijibu hoja iliyotolewa na msanii Christian Kauzeni ambaye alitaka kujua ni
kwa nini wasanii wakongwe wengi wanakuwa na maisha magumu licha ya kuwa
walifanya kazi nzuri zilizo wahengea umaarufu mkubwa hapa nchini.
Alisema wasanii wengi
wakonge hawakuwa na utaratibu wa kuweka akiba, lakini kwa sasa kuna mifuko
mingi na mifumo mingi ya kujiwekea akiba hivyo ni muhimu kwa sanii kujiwekea
akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema huu si wakati wa msanii kupata
shida baada ya kustaafu au kuzeeka kwa kuwa kuna mifuko mingi ya kuweka akiba
na hata ya huduma za afya ambayo kwa mchango kidogo inatoa unafuu mkubwa
wahuduma.
“Haipendezi kwa msanii aliyekuwa
na jina kubwa au umaarufu katika nchi anapokuwa amepatwa na maradhi kusubili harambee
ipite ili apate matibabu, msanii akijiunga na mfumo wa bima ya Afya kwa mfano NHIF
analipa fedha kidogo sana na anapata uhakika wa matibabu kwa muda mrefu wa maisha
yake,” alisema Mngereza.
No comments:
Post a Comment