Meneja wa timu ya Coastal Union, Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal Union winga mpya wa Kulia, Ibrahim Twaha "Messi" mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
Winga wa kulia Mpya wa Coastal Union Ibrahim Twaha "Messi" akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Coastal Union kulia ni Katibu Mkuu,Kassim El Siagi kushoto ni Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai.
NA MWANDISHI WETU, TANGA
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kufanya usajili wa nguvu ili kujiimarisha vilivyo katika safu mbalimbali ambapo jana ilifanikiwa kuingia mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili aliyekuwa winga wa kulia wa Simba,Ibrahim Twaha “Messi”
Utiliaji saini wa mkataba huo ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mjini hapa na kushuhudiwa na viongozi waandamizi akiwemo Katibu Mkuu Kassim El Siagi na Meneja wa timu hiyo,Akida Machai.
Akiuzngumza mara baada ya kumalizika utiaji saini huo,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao hasa anapokuwa uwanjani .
Alisema kuwa winga huyo ana vitu adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa maendeleo timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
“Niseme tu safari hii tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara na hili tunalifanya kuhakikisha tunarudisha kombe mkoani hapa ambalo tulilichukua mwaka 1988 “Alisema El Siagi.
Kwa upande wake,Ibrahim Twaha “Messi”mara baada ya kusaini mkataba huo alihaidi kuipa mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika safari za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Sasa ni kama nimerudi nyumbani kwa sababu awali nilikuwa naitumikia timu hii hivyo najisikia faraja kubwa kurudi tena Coastal Union mi nihaidi kushirikiana nao kwa lengo la kuipa mafanikio “Alisema Messi.
Awali akizungumza,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiri kufanya usajili nzuri ambao utaiwezesha kutwaa ubingwa na kurudisha makali yao ya miaka ya nyuma.
No comments:
Post a Comment