Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuanza kesho Jumanne kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa kwanza utakua ni kati ya Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya Rwanda itakayotoshuka dimbani saa 7:45 mchana kucheza na vijana wa Kwesi Appiah timu ya Al Khartoum kutoka nchini Sudan.
Saa 10:15 kamili jioni, Gor Mahia mabingwa wara tano wa michuano ya Kagame watashuka dimbani kucheza na Malakia kutoka Sudan Kusini, viingilio vya michezo hiyo ya jumanne cha chini kitakua ni elfu tatu (3,000) na kiingilio cha juu kitakua ni elfu kumi na tano (15,000).
Robo fainali zitaendela siku ya jumatano, ambapo michezo miwili itachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku macho na masikio ya wapenzi wa mpira Afrika Mashariki yakielekezwa kwa mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Kabla ya mechi hiyo ya wapinzani wa soka nchini Tanzania kuchezwa majira ya saa 10 jioni, mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy kutoka nchini Sudan.
Viingilio vya mchezo wa siku ya jumatano, kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilo cha juu kitanua ni elfu ishirini (20,000).
Katika hatua hiyo ya robo fainali endapo timu zitacheza kwa dakika 90 na mchezo kumalizika kwa sare, hatua itakayofuata ni kumpata mshindi kwa matuta (penati).
No comments:
Post a Comment