NA DEGE MASOLI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewatangaza makada watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge wa majimbo manne ya mkoa wa Tanga.
Waliopitishwa kupambana na CCM ni David Chanyeghea, Jimbo la Bumbuli lililokuwa likiongozwa na January Makamba ambaye amechukua fomu kutetea tena nafasi yake.
Chanyeghea amepitishwa jana na mkutano mkuu maalumu wa kura za maoni uliyofanyika mjini Bumbuli baada ya kupata kura 67 na kuwabwaga wenzake watatu waliyokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Katika jimbo la Mkinga walimpitisha Recho Sadick kupeperusha bendera ya Chadema baada ya kupata kura 103 kati ya 104 zilizopigwa na moja kuharibika.
Atakayeipeperusha bendera ya chadema Jimbo la Korogwe vijijini ni Emanuel Kimea baada ya kuwabwaga wapinzani wake wanne wakati Korogwe mji ni Aman Kimea aliyewashinda wapinzani wake sita.
Wakati huo huo, makada 25 wa CCM wamejitokeza kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo ya Kilindi na Lushoto.
JIMBO LA KILINDI
Makada 15 akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kilindi, Beatrice Shellukindo, wamejitokeza kuwania jimbo hilo.
Mwingine ni aliyekuwa mbunge wa kwanza wa jimbo hilo, Juma Kidunda, Aisha Kigoda, Said Mkindawantu, Hemed Magati, Keleni Mngoya, Msilagi Shaban, Kingazi Kilua na Majiyablulu Grenford.
Makada wengine ni Kimweri Mohamed, Rashid Madeni, Athuman Rusewa, Magawa Ndaro, Juma Mgaza, na Ally Kidunda.
JIMBO LA BUMBULI
Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Bumbuli, January Makamba (CCM) amepata upinzani kutoka kwa makada wawili wa chama hicho, Bakar Mshihili na Abdulkadir Kaniki baada ya kuchukua fomu na kuzirejesha nao wao wakiomba ridhaa ya kuipeperusha bendera katika nafasi ya ubunge.
JIMBO LA LUSHOTO
Henry Shekifu amepatawapinzani 10 makada waliyojitokeza kukabiliana na Shekifu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Tanga ni Hamida Kilua, Abdul Mshangama, Riziki Shemdoe, Nyero Hizza, Paulina Jandwa, Prof Vicent Kihiyo, Evelini Kweka, Emile Sisili na Shaban Bozinia.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment