Mabaki ya ndege yaliyopatikana Mashariki mwa Madagascar
Serikali Nchini Australia imeelezea kupatikana kwa kipande cha mabaki ya ndege "kama hatua muhimu" katika utafutaji wa ile ndege ya Malaysia iliyotoweka ya MH-370.
Malaysia imetuma kundi la wataalamu kuthibitisha iwapo mabaki ya ndege yaliyogunduliwa katika kisiwa cha Reunion Mashariki mwa Madagascar ni mabaki ya ndege iliyopotea ya shirika la ndege la Malaysia nambari MH370.
Naibu waziri wa uchukuzi wa Ufaransa Abdul Aziz Kaprawi, amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa mabaki hayo ni ya ndege aina ya Boeing triple-seven, muundo sawa na ile ya ndege ilitoweka angani.
''Kila sehemu ya ndege huwa na nambari maalum'' alisema afisa mmoja.
''Hiyo ndio itakayotusaidia kutambua hata kutoka kwa mabaki baada ya ajali.''
Hakuna ndege yoyote chapa Boeing triple-seven ambayo imewahi kuanguka katika maeneo hayo ya kusini mwa sayari ya dunia.
Shuguli za kuitafuta ndege hiyo ilienga zaidi kilomita elfu sita Mashariki zaidi, lakini viongozi nchini Australia wanasema kuwa huenda mabaki hayo yilisombwa na maji kutoka huko.
Watu wote mia mbili na thelathini na tisa waliokuwa wakisafiri kwenye ndege hiyo, walipoteza maisha yao.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment