Uhispania imeongeza umri wa ndoa kutoka miaka 14 hadi 16 , ikiwa ni nchi iliyoidhinisha umri wa chini zaidi wa kuolewa barani Ulaya.
Kabla ya kupandishwa kwa miaka, wavulana na wasichana wangeweza kuolewa wakiwa na miaka 14kwa ruhusa ya hakimu.
Mabadiliko hayo yamekuja miezi kadhaa baada ya serikali kuongeza miaka ya idhini ya kuolewa kutoka miaka 13 hadi 16.
Serikali ilitangaza azma yake ya kufanya marekebisho ya sheria mwezi Aprili 2013, lakini mabadiliko hayo yameanza kutekelezwa leo Alhamisi.
Hatua hiyo imeafikiwa na maafisa kutoka shirika la watoto duniani Unicef na makundi ya haki za watoto nchini Uhispania.
Kwa mujibu wa gazeti la El Pais (nchini Uhispania), ni ndoa 365 zilizowahusisha wavulana na wasichana wa chini ya miaka 16 zilizofungwa kati ya mwaka 2000 na 2014 - huku tano tu zikifungwa mwaka 2014.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment