Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 6 December 2014

WATU 5,000 WAZUIWA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza

Ikiwa imebaki wiki moja kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, wananchi zaidi ya 5,000 wa jamii ya wakulima na wafugaji wilayani Bagamoyo wamezuiwa kupiga kura baada ya kuzuka mtafaruku katika zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Mpiga kura.


Hatua hiyo, inafuatia Mtendaji wa Kata ya Tarawanda, Masoud Chabo, kuhamishia kituo cha uandikishaji nyumbani kwake kwa madai kuwa sheria mpya ya uchaguzi ya mwaka huu, inawataka watendaji kupanga vituo vipya, hali iliyowafanya wafugaji hao kugoma.

Wafugaji hao wa kijiji cha Magurumatari Kata ya Tarawanda, Wilaya ya Bagamoyo, wamedai kuwa kituo hicho kipya kipo mbali na makazi yao kitendo kitachosababisha washindwe kwenda kupiga kura.

Akifafanua, Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Magurumatari, Chabo, alisema Sheria ya uchaguzi ya mwaka 2014, inawataka viongozi na watendaji wahakikishe wananchi wanajiandikisha katika kata zao.

Alisema alihamishia kituo cha kujiandikishia nyumbani kwake lakini wafugaji hao wameng'ang'ania pale wanapojiandikishia na kupigia kura miaka yote, jambo ambalo haliwezekani kwani sheria lazima zifuatwe.

Mwenyekiti wa Kata hiyo, Ramadhani Athumani, alisema idadi ya wafugaji na wakulima ni 5,000 na hawakuweza kuandikishwa kwenye daftari hilo kutokana na  kuzuka malalamiko.

Alisema uongozi umeamua watu hao wasipige kura mpaka uchaguzi utakapomalizika ndipo viongozi watakaa kusikiliza matatizo yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulich Matei, alisema kuwa taarifa za vurugu hazijafika ofisi kwake ila anajua kuna mgogoro wa kisiasa ambao unatakiwa ushughulikiwe ili kuepusha mapigano yanayoweza kutokea.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, alisema atamtuma msimamizi wa uchaguzi aende akawape maelekezo ili mambo ya ugomvi yaishe na wakazi hao waishi kwa amani.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na NIPASHE, wakazi hao walisema wameamua kuandaa ulinzi wa jadi baada ya mwenzao mmoja kutishiwa kuuawa na jamii ya wakulima ambao wamedai wanapewa kipaumbele cha kuishi eneo hilo.

Mwenyekiti wa wanawake Magurumatari, Magdalena Sambo, alisema awali walikuwa wakiishi katika kijiji hicho bila kupata usajili lakini mwaka 2009 walipewa na kupangiwa makazi yao kati ya wakulima na wafugaji na kila kundi lilipata hekta 300.

“Haitawezekana tusipige kura, kama sisi hatupigi na hawa wakulima hawatapiga, maana wote tupo hapa tangu mwaka 1999 mpaka tumeshughulikia kusajiliwa kwa kijiji mwaka 2009, iweje leo kituo chetu kihamishwe na sisi tukataliwe kujiandikisha hapa uchaguzi hautafanyika,” alisisitiza.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment