
Umati wa watu katika mojawapo ya mikutano ya Chama cha Mapinduzi
Na Hastin Liumba,Tabora
WANACHAMA wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) kata ya Tumbi mkoani Taborawametishia kukihama chama hicho na
kujiunga na vyama vya upinzaniwakidai kuchoshwa na viongozi wa CCM kata ambao
wamekuwa wakiwagawakwa misingi ya udini na ubinafsi.
Kwa nyakati tofauti wakiongea na waandishi wa habari katika kata yaTumbi Manispaa walisema wamekuwa wakitengwa kwa kuwa wao ni wakristona kwamba wananyimwa fursa ya kushiriki kwenye mambo ya kukijengachama.
“Tunatengwa sana eti sisi ni wakristo... mbaya zaidi viongozi wetu niwabinafsi tunafikiria kukihama chama muda wowote.”
Aidha wanachama hao walisema viongozi wa CCM kata ya Tumbi wenyematatizo na wamewagawa wanachama ni diwani wa kata hiyo HamisMuhogo,mwenyekiti wa CCM kata ya Tumbi Seif Ramadhani Mbalamwezi nakatibu kata wa CCM Maulid Hamis.
Walisema wamefikia mahali wamechoshwa na hali ya ubinafsi na kutengwakwa misingi ya kidini na sasa wanawaza kuondoka ndani ya CCM iliwapate fursa ya kutumia nafasi zao kwenye siasa na hata kutafuta amani nje ya CCM.
Aidha waliomba uongozi wa chama mkoa wa Tabora kuja katani hapo nakuongea na wanachama wa CCM ili ukweli ujulikane jinsi chama kilivyona sura ya kubaguana.
Diwani wa kata ya Tumbi Hamis Muhogo alipoulizwa juu ya shutuma hizialikana na kusema ni fitna za kisiasa.
Kwa upande wao mwenyekiti wa CCM kata ya Tumbi Seif RamadhaniMbalamwezi na katibu kata wake Maulid Hamis walikana tuhum zao nakusema hawajui kama kuna madai ya kuwepo mgogoro na wanachama wao.
Hata hivyo walisema wanachama wanaoleta malalamiko yao walishindwakwenye kura za maoni kuelewa uchaguzi vijiji.
Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bakar Luasa alikiri kupokea malalamiko hayo na ataenda kutatua mgogoro huo siku ya Jumatano.
No comments:
Post a Comment